Ndugu Wanajumuiya wa Minnesota/New York,
Sisi watoto na familia ya Mama Lulu Mwaluko, tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kwa jumuiya za watanzania za Minnesota na New York, kwa msaada mkubwa wa hali na mali, na mapenzi mliyotuonyesha katika kipindi kifupi cha kumuuguza, mpaka mauti ya mama yetu mpendwa, Lulu J.M. Mwaluko aliyefariki March 7, 2014 katika hospitali ya Calvary huko Bronx, New York.
Kwa kweli hakuna maneno yanayoweza kuelezea jinsi tulivyofarijika kwa uwepo wenu kati yetu katika kipindi chote cha msiba, ila tunaomba mpokee salamu hizi kama ishara ya shukrani zetu kwenu nyote:
- Wanajumuiya wa New York, mlituonyesha ushirikiano mkubwa haswa katika maandalizi ya kumuaga marehemu kule Mount Vernon, NY; na pia katika kukamilisha mipango ya kumsafirisha mama yetu kuelekea Moshi, Kilimanjaro ambako marehemu sasa amepumzika katika mji aliozaliwa.
- Wanajumuiya wa Minnesota ambao ingawa hamkuwa nasi jimboni New York, tunashukuru kwa kuwa nasi kiroho, na misaada ya hali na mali.
- Bila kuwasahau Ubalozi wa Tanzania-NY ambao walikuwa nasi bega kwa bega katika kukamilisha zoezi zima la kumpeleka mama yetu kwenye pumziko lake la milele.
- Mwisho tunapenda kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki wengine wote popote pale walipo, ambao pia walikuwa pamoja nasi kwa karibu sana, na kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu.
Mungu andelee kuwabariki sana, na kuwa pamoja nanyi nyote ili muendeleze ushirikiano na upendano kama mlivyotuonyesha.
Wenu,
Emma Kasiga
Mwanajumuiya wa Minnesota,
K.N.Y. Watoto na Familia nzima ya Marehemu Mama Lulu Mwaluko.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...