![]() |
MAREHEMU MOSHI CHANG’A |
Bismillah Rahmani Rahim
Familia ya akina MWACHANG’A wa Iringa
inatoa shukurani za dhati kwa ndugu jamaa na marafiki wote walioshiriki kwahali
na mali kuanzia kumuuguza mpaka kufanikisha mazishi ya mpendwa wao marehemu MOSHI CHANG’A aliyefariki siku ya Jumapili
tarehe 20.04.2014 katika hospitali ya Muhimbili na kuzikwa Kihesa mkoani Iringa
Mjini katika makaburi ya Mtwivira, siku ya Jumatano tarehe 23.04.2014.
Aidha shukurani za pekee zimuendee
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa faraja kubwa aliyoitoa toka kumuuuguza
marehemu mpaka alipofariki na kuzikwa.
Shukurani za dhati zimuendee Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Peter
Pinda (Mb) kwa nasaha zenye faraja kubwa alizozitoa katika kipindi chote kuanzia
kuuguza na nasaha alizozitoa wakati wakuaga
mwili wa marehemu pale Mbagala.
Shukurani nyingi kwa Mh. Waziri Hawa Ghasia, mawaziri na makatibu wakuu wote walioshiriki na kutufariji
katika msiba huu.
Tunawashukuru mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam Mh. Said Meck Sadick, Mkuu wa mkoa wa Rukwa
Eng. Stella Manyanya, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na mwenyeji
wa mazishi Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Tunawashukuru zaidi Viongozi wote wa serikali wakiwemo
Mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na Madiwani wa wilaya zote
walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kipindi chote cha kuuguza mpaka
mazishi ya marehemu.
Aidha shukurani za pekee zimuendee Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda kwa faraja kubwa aliyoitoa kwa
wafiwa hasa siku ya mazishi pale Iringa mjini, Mbunge wa Iringa Mjini na wabunge
wote waliotufariji kwahali na mali ahsanteni sana
Mstahiki Meya wa mji wa Iringa Mh. Mwamwindi,
viongozi wote wa vyama vya siasa na serikali wangazi zote mkoani Iringa, Mashehe walioongoza na kusimamia mazishi
na viongozi wadini mbalimbali walioshirikiana nasi kwenye msiba huu tunawashukuruni
sana.
Aidha shukurani za pekee ziwaendee Madaktari na wauguzi
wote wa hospitali ya Muhimbili kwa tiba nzuri na juhudi kubwa walizofanya ili kuokoa
maisha ya marehemu katika kipindi chote cha kuugua kwa marehemu nasema ahsanteni
sana
Hakika sirahisi kumtaja kwajina kila mmoja wenu,
aliyetufariji na kutusaidia kuanzia kipindi cha ugonjwa, mazishi mpaka baada yamazishi,
lakini fadhila zenu kamwe hazitosahaulika, na kwamba shukurani zetu zimfikie kila mmoja wenu
na kwamba tunamuomba Allah Subhana Wataalah
awalipe yaliyo mema hapa duniani na kesho akhera In Shaa Allah.
Mwisho tunaishukuru
serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kwa misaada, faraja na ushirikiano
mkubwa iliotupatia katika kipindi chote cha tiba, mazishi na mpaka baada ya mazishi.
INA LILLAHI WA INNA
ILAIHI RAAJIUN
Familia
ya Wafiwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...