Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Afrika (katikati), akiongoza mjadala huo ambao ulihudhuriwa pia na Bibi. Leila Zerrougui ( wa tatu kushoto), Mwakilishi Maalamu ( Special Representative) wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya watoto na Vita, na Balozi Smail Chergui (wa nne kushoto), Kamishina wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika. Aliopo nyuma ya Mhe. Balozi Naimi Aziz, ni Bi. Suma Mwakyusa, Afisa Ubalozi Mwandamizi.
Bw. Samwel Shelukindo, Afisa Ubalozi Mkuu, akitoa mchango wa Tanzania katika mjadala huo, ambao pamoja na mambo mengine, Tanzania ilisisitiza umuhimu wa kuingozea nguvu (mandate) mahakama ya Afrika inayoshughulia masuala ya haki za binadamu ( African Court on Justice and Human Rights) ili iweze kuwashughulikia watu wanaotenda uhalifu dhidi ubinadamu katika vita ikiwemo kuwatumua watoto vitani. Aliopo nyuma ya Bw. Shelukindo ni Bw. Nsavike Ndatta, Afisa Ubalozi Mkuu akifuatilia mjadala huo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini mjadala huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...