Na Luteni Kanali Juma Sipe 
(PA, Marekani). 
 Jeshi la Wananchi (JWTZ) limeshiriki Mkutano wa Baraza la Michezo la Kimataifa (General Assembly and Congress of the International Military Sports Council -CISM) uliofanyika Mjini Quito, Equado America ya Kusini kuanzia tarehe 05-09 Mei, 2014.
 Mkutano huo ulijadili na kuendelea kusikilizana ushiriki wa majeshi katika Michezo ya Kimataifa chini ya Kaulimbiu ya Baraza hilo isemayo Urafiki kupitia Michezo (Friendship through sports), msisitizo ukiwa katika kutumia michezo kama chombo cha kueneza amani na utulivu kati ya mataifa duniani. 
Badala ya kukutana na kushirikiana katika maeneo ya vita na migogoro, majeshi yakutane katika michezo na kujenga uelewano na mashirikiano yatakayopunguza uwezekano wa kuingia katika vita kama njia ya kutatua migogoro. 
 Moja ya mambo yaliyojitokeza katika mkutano huo ni pamoja na ushiriki mdogo wa nchi za Afrika ikilinganishwa na mabara mengine, uliodaiwa kutokana na kukosekana fedha, mwamko mdogo wa viongozi wa majeshi ya nchi husika na kutoona umuhimu wa kujenga mahusiano kupitia michezo. Aidha, Mkutano ulimchagua pia Rais mpya wa Baraza hilo, Kanali Abdul Hakeem kutoka Bahrain na Kanali Dorah Mumby (Guinea) kuwa Katibu Mkuu wa kwanza kutoka Afrika. 
 Ushiriki wa Tanzania na utekelezaji wa maazimio ya CISM umekuwa wa mfano kwa miaka kadha sasa. Kwa mfano, katika mkutano wake wa mwaka 2008 uliofanyika Paramaribo, Suriname, Meja Joseph Bakari (sasa Luteni Kanali) alitunukiwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza hilo Nishani iitwayo ‘Order of Grand Knight’ kwa mchango wake uliopelekea kuanzishwa kwa “Twalipo Youth Sports Foundation” (twalipo soccera cademy.blogspot. com) nchini Tanzania. 
 Katika mkutano huo jumla ya wanachama 76 walihudhuria kati ya wanachama 104 wa Baraza hilo. Tanzania iliwakilishwa na Kanali Martin Busungu, Mkurugenzi wa Utimamu wa Mwili, Michezo na Utamaduni kutoka Makao Makuu ya Jeshi na Luteni Kanali Joseph Bakari, Afisa mnadhimu kutoka Kurugenzi hiyo.
 Mkutano huo wa mwaka hutanguliwa na mikutano ya kimabara (Afrika, Ulaya, Asia na Amerika) ambako masuala ya michezo ya Majeshi yanayogusa mabara husika hujadiliwa. 
 Kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika  nchi zilizoshiriki ni pamoja na Kenya, Uganda na Zambia. 
 Kwa uelewa zaidi tafadhali tembelea wavuti www.cismmilsport.org











 Ujumbe wa Tanzania Kanali Martin Busungu (kushoto) na  Luteni Kanali Joseph Bakari wakati wa mkutano.
 Kanali Busungu akipiga kura wakati wa uchaguzi wa viongozi wapya ya Baraza.
 Luteni Kanali Bakari akichangia mada wakati wa Mkutano.
 Kanali Busungu akiteta jambo na Mkuu wa Ujumbe wa Kenya, Brigedia Jenerali Lipakio wakati wa mapumziko.
  Meja Bakari (sasa Luteni Kanali) wakati akitunukiwa nishani mwaka 2008.
Ujumbe wa Tanzania ukiinua bendera juu kuashiria uwepo wao mkutanoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...