Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akijiandaa kuwasilisha mchango na maoni ya Tanzania wakati wa Mkutano wa kumi na Moja wa Kikundi Kazi cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Kikundi Kazi hicho ambacho Tanzania ni mjumbe kilikutana wa wiki moja ambapo kilipitia na kuboresha rasimu ya malengo mapya ya maendeleo baada ya 2015. Walio kaa nyuma wa Balozi ni Dr. Lorah Madete, Afisa Mkuu kutoka Ofisi ya Rais-Tume ya Mipango na Bw. Noel Kangada Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu.
Dr. Lorah Madete akimpongeza mmoja wa Mwenyekiti- Mwenza wa Kikundi Kazi Mwakilishi wa Hungary Balozi Csaba Korosi mwishoni wa mkutano wa 11 wa kikundi kazi hicho. Pembeni anaonekana Mwakilishi wa Kenya, Balozi Macharia Kamau ambaye pia ni Mwenye Kiti- Mwenza wa kikundi hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...