Jiji la Abuja, ambao ndilo makao makuu ya nchi ya Nigeria, lipo katikati ya nchi hiyo kubwa na tajiri yenye utajiri mkubwa wa mafuta na gesi. Mji huu ulijengwa miaka ya 1980, na ukatangazwa rasmi kuwa makao makuu ya nchi December 12, 1991, kuchukua nafasi ya jiji la Lagos, ambalo linabakia kuwa ni jiji lenye wakazi wengi kuliko sehemu yoyote katika Nigeria.
Kama ilivyo ada, Abuja limekua siku hadi siku huku likishuhudia ongezeko kubwa la watu kiasi cha serikali kulazimika kuanza kujenga miji ya pembeni (satellite cities) katika maeneo ya Karu, Suleja, Gwagwalanda, Lugbe, kuje na sehemu zingine ndogondogo ambako mji huo unaelekea.
Inakadiriwa mji wa Abuja una wakaazi takriban milioni tatu, hivyo kuwa mji wa nne wa Nigeria wenye wakaazi wengi, wa kwanza ukiwa Lagos (milioni 21), Kano na Ibadan. Inasemekana mwaka 2006 Lagos ilikuwa na watu milioni 17.5, kwa mujibu wa sense iliyofanyika mwaka huo. Kwa sasa, ongezeko la watu likiwa asilimia 3.2 kwa mwaka, jiji hilo sasa lina wakaazi milioni 21.
Kwa Tanzania, jiji la Dar es salaam lina wakaazi 4,364,541 kwa mujibu wa matokeo ya sense ya watu na makaazi ya mwaka 2012.
Jiji la Dar liliacha kuwa na hadhi ya makao makuu ya nchi mwaka 1974, na mji wa Dodoma kuchukua nafasi hiyo.
Historia ya mji wa Abuja inaanza miaka ya 1970 wakati wa migogoro ya kidini na kikabila ilipokuwa kileleni. Ndipo mikakati ikawekwa kuwa na makao makuu ya nchi katikati ya nchi ambapo patakuwa huru na rafiki kwa kila upande unaopingana.
Sababu ingine ya kuhamishia makao makuu hapo Abuja ambako awali palikuwa na kijiji kidogo na misitu, ni msongamano kutokana na wingi wa watu katika jiji la Lagos.
Mpango uliotumika ni kama ule wa Brazil ambao walichagua kujenga makao makuu yake Brasilia, kutoka Rio de Janeiro. Jiografia ya Abuja inajengeka kuanzia mwamba mkubwa uitwao Aso Rock, wenye ukubwa wa mita 400.
Mji huu pia una sifa za kuwa mji uliopangika kwa ubora wa hali ya juu , tajiri na ghali sana kuishi barani Afrika.
Nimeangalia picha zote kwa kweli nimekubali Abuja iko poa. Lakini ni vizuri tukajifunza kuwa jiji kuwa zuri na la kuvutia ni pamoja na wasanifu majengo na miji kwa ujumla kuwa wabunifu, pili wananchi kuwa na hulka ya kufuata sharia (mfano kuotupa taka ovyo, kutovukia sehemu ambazo haziruhusiwi kuvukia, kuheshimu miuondombinu n.k.), tatu viongozi kuacha ufisadi ili pesa zitekeleze miradi mikubwa na nne usimamizi mzuri wa sheria.
ReplyDeleteMasjid nzuri sana mashaallah
ReplyDeleteNi taswira nzuri na ni mji uliopangwa vizuri
ReplyDeleteWenzetu naona watuzidi Ujanja kazi yetu sie ni kukata mataputapu tu.
ReplyDeleteMji umetulia lakini ukumbuke kuna Boko huko si masihara. Yaani kipindi chote cha mkutano ofisi zote za umma na serikali zimefungwa na shule zimefungwa ili kuimarisha ulinzi.
ReplyDeleteKumbe hata morogoro inawezekana
ReplyDeleteThe mdudu,ndugu zangu watanzania msije mkapotea kozi kwenda kwenye hiyo miji yao NJAA mtu na pia wanaongoza kwa wizi DUNIANI na pembezoni mwa hiyo miji hakiyamungu huwezi fananisha na miji yetu yenye neema tele ila kwao watu wanasurubika kama unavyoona INDIA,kwetu Tanzania nimeshatembelea Mikoa yote na sijawahi kuona watanzani wakiishi juu ya maji na viboti vya ajabu lakini Lagos na Abuja na India hivyo vitu kwao ni sehemu kubwa ya maisha yao.
ReplyDeleteDodoma si makao makuu ya nchi Tanzania.
DeleteVipi mafuriko huko hakuna ankal?
ReplyDeleteHuwezi kufananisha Tanzania na Nigeria na India hao wako mabilioni ya watu ndio maana hawana sehemu za kuishi.Na sisi tunaenda huko huko.Zamani mtaa wa Samora ulikuwa msafi lakini siku hizi ni kama mtaa wa Kongo watu kibao kila mtu anataka kuishi Dar.
ReplyDeleteMdau uliyesema Nigeria wana shida nyingi kuliko sisi watanganyika hebu jiulize kama wana shida kwa nini vimiji vyao vinapendeza? Kwa nini sisi tusio na shida inakuwa taaaaabu kuupendezesha mji? Hebu angalia Dar ambayo ni sebule ya Tanzania ilivyokuwa chafu. Nyumba zimepangiliwa hovyo hovyo tu hata hazivutii. Hata kusafisha jiji imekuwa tabu? Hata watu kuheshimu miundombinu inakuwa tabu?
ReplyDeleteThe mdudu acha kujiliwaza. Tanzania tuna mengi ya kujifunza kutoka nchi nyingi za Afrika. Mbali na matatizo waliyonayo hawaachi kuendelea. Kwetu hatuna matatizo hayo lakini pamoja na amani zikiwemo laslimali kibao, maendeleo ya kutafuta kwa darubini. Tuchape kazi tuache longolongo. Michuzi unafanya jambo la maana sana kutuonesha nchi nyingine tena za Afrika zinavyopiga hatua. Tutumie changamoto hizi kujiimarisha zaidi.
ReplyDeletewadau tusiwe wabishi bila Mantiki,leo hii Maendeleo yaliyopo India nchi yenye watu 1.2 bilioni ni ya mbali sana na hatuwezi jilinganisha na sisi Tanzania.hata chembe.
ReplyDeleteMdau unayesema nchi kama India na Nigeria zina shida unashindwa kuelewa kila mahali pana shida zake. Mbona sisi tunapeleka wagonjwa wetu kwao ka matibabu kama wangekua na shida si wangekuja kwetu kwa hizo huduma? Tukubali na tujifunze kutoka kwao kwanini wao na shida zao wanaweza kuendelea na sisi pamoja na amani na rasimali tele nini kinatukwamisha hata hatuwezi kufagia mitaa yetu au kuzibua mifereji ya maji machafu.
ReplyDelete