Wakuu wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakizindua kitabu rasmi cha Muongozo wa Majaji wa Jumuiya hiyo kwenye Mkutano wa 12 wa siku moja wa Jumuiya hiyo uliofanyika ukumbi wa Kimataifa wa Arusha.  Rais Uhuru Kenyata wa Kenya ambae ndie Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni pamoja na Mwenyeji wa Mkutano huo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Wengine ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Burundi Bwana Bazombasa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyemuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohd Sheni pamoja na Waziri Mkuu wa Rwanda Bwana Pierre Damieni Habumuryemi.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba yaRais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Sheni akipokea kitabu wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mkoani Arusha.
 Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania waliohudhuria Mkutano wa 12 wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki huko Arusha. Wa mwanzo kutoka kushoto ni Waziri wa Ardhi wa SMZ Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mh. Benard Membe na Waziri wa Afrika Mashariki Mh. Joh Samuel Sitta. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2014

    ...kumbe Zanzibar ni nchi!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2014

    Ukweli wa mambo hali ya hewa ktk nchi mbili ndogo za Afrika ya Mashariki si shwari ndio maana Wakuu wake hawakufika Arusha jana.

    Wanaogopa Kupinduliwa kama watatoka nje ya nchi huku mmoja akibakia Jijini KG na huku akitengeneza safari ya Kisanii kugeresha kama yupo safarini California-Marekani!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2014

    Jumuia iimarishwe kwa manufaa na maendeleo ya watu wa ukanda huu wa Afrika.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 02, 2014

    Mdau wa No.1 ndio Zanzibar ni nchi na MUUNGANO upo palepale!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 02, 2014

    Mdau wa 3 la muhimu Jumuia ifuate matashi wa wananchi wa nchi husika na sio matashi ya viongozi wao tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...