Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuanzia msimu wa 2015/2016 itakuwa na timu 16 badala ya 14 za sasa.

Mabadiliko hayo yamepitishwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Mei 3 mwaka huu) jijini Dar es Salaam baada ya kupokea mapendekezo ya kuongeza idadi ya timu kutoka kwenye Kamati ya Mashindano.

Uamuzi huo umefanywa kwa lengo la kuongeza ushindani katika ligi hiyo, na kuwezesha wachezaji kupata mechi nyingi zaidi za mashindano. Kwa mabadiliko hayo maana yake ni kuwa Ligi ya msimu wa 2015/2016 itakuwa na mechi 240 wakati kwa sasa ina mechi 182.

Kuhusu idadi ya wachezaji wa kigeni kwenye VPL, Kamati ya Utendaji itafanyia uamuzi mapendekezo katika eneo hilo baada ya kwanza kupata maoni ya klabu za VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambazo Mei 11 mwaka huu zitakutana na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Mapendekezo ya Kamati ya Mashindano ni kuwa idadi ya wachezaji wa kigeni iendelee kuwa watano kama ilivyo katika kanuni za sasa za VPL.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2014

    Hongereni sana TFF.Pamoja na ugumu wa fedha si vibaya zikafika timu 20.Washawishini TRA watuletee timu,ili nayo iwe inalipa KODI!(Utani).Wenzao wa Uganda wanayo(URA).Kampuni za BIA,SIGARA nk zifikirie tena kuanzisha vilabu vya SOKA kama ilivyokuwa zamani.

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...