Na Mwandishi Maalum

Touch Foundation , Taasisi isiyo ya kiserikali na yenye makao yake nchini Marekani, mwishoni mwa wiki (Mei 8), imeadhimisha miaka kumi ya kazi zake na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania na Taasisi nyingine katika uboreshaji na uimarishaji wa sekta ya afya nchi.

Katika hafla iliyojulikana kama Asante Supper 2014, ilihusisha pia utoaji wa tuzo kwa wadau mbalimbali ambao wamekuwa nguzo muhimu ya Taasisi hiyo. Asante Supper ilihusisha pia harambee ya uchangishaji wa fedha kwaajili ya kusaidia sekta hiyo ya afya. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Morgan Library Museum, Jijini New York.

Akiwakaribisha wageni waalikwa, Rais wa Touch Foundation, Lowell Bryan pamoja na kuelezea mafanikio ya taasisi yake iliyoanzishwa mwaka 2004 katika uboreshaji wa sekta ya afya nchini Tanzania, amewataka wafadhili mbalimbali kuendelea kujitolea na kuchangia zaidi ili sekta ya afya nchini Tanzania iweze kuimarika na hatimaye kumaliza au kupunguza changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo.

Akasema utashi wa kisiasa na wa kiuongozi ambao Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameonyesha katika, si tu kutambua na kuthamini mchango wa Touch Foundation na Taasisi nyigine kama hiyo, bali pia amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba sekta ya afya inaimarika nchini Tanzania na huduma za afya zinawafikia wananchi kule walipo.

Naye Padre Dkt. Peter le Jacq ambaye naye amekuwa na mchango mkubwa wa uimarishaji wa sekta ya afya nchini kupitia Hopistali ya Buganda ana ambaye haswa ni chimbuko la Touch Foundation, hakusita kutoa shukrani zake kwa Rais Kikwete na kumuelezea kama kiongozi anayejituma, kujitolea na mwenye ushirikiano mzuri za sekta binafsi.

Katika Miaka kumi ya uhai wake Touch Foundation imekuwa ikishirikiana na kufanya kazi kwa Karibu na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, na hususani Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afya na Sayansi Mwambata cha Bugando (CUHAS). Ushirikiano huo unahusisha katika maeneo mbalimbali mtambuka yakiwamo mafunzo ya madaktari na wataalam wa fani mbalimbali kupitia CUHAS na hivyo kuchagia ongezeko la madaktari na wataalam.

Mbali ya watendaji wakuu wa Touch Foundation, wakiongonzwa na Rais wake, Bw. Lowell Bryan, pamoja na wafadhili.Asante Supper 2014 ilihudhuriwa pia na wageni maalum kutoka Tanzania na ujumbe huo ulihusisha Muhashamu Thaddaeus Ruwa’ichi Askofu Mkuu wa Mwanza na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,Balozi Tuvako Manongi alikuwa miongoni wa wageni waaalikwa.

Wengine kutoka CUHAS walikuwa ni Askofu Augustine Shao, Makamu Mkuu wa CUHAS ,Profesa Jacob Mtabaji, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, Padre Dkt. Charles Kitima, Profesa Paschalis Rugarabamu, Dkt, Isidor Nyahomela, Dkt. Frederick Kigadye, Dkt. Charles Majinge, Dkt. Manage Manyama, Dkt. Stella Mongella, Dkt. Godwin, Godfrey Sharau na Sister Marie- Jose Voeten kutoka hospitali Teule ya Sengerema.

Baadhi ya Madaktari hao kutoka Bugando na hasa wale walionufaika na ufadhili wa Touch Foundation walielezea walivyonufaika na ufadhili huo ambao umewawezesha kusoma, kujipatia ujuzi na hivyo kupata fursa ya kuwahudumia watanzania wenzao.
Rais wa Touch Foundation, Bw. Lowell Bryan akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa na Mke wa Balozi, Bibi Upendo Manongi wakati wa Hafla ya Asante Supper 2014 iliyofanyika mwishoni mwa wiki, hafla hiyo ilikuwa ni kuadhimisha miaka 10 ya Taasisi hiyo iliyokwenda sambamba na harambee ya kuchangia uimarishaji wa sekta ya Afya nchini Tanzania. Touch Foundation inafanya kazi kwa karibu na Serikali ya Tanzania na Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki cha Afya na Sayansi Mwambata ( CUHAS) Bugando Tanzania. Katika hafla hiyo, ambayo ilihudhuriwa na Viongozi wa CUHAS wakiongozwa na Mhashamu Askofu Mkuu, Yuda Thaddaaeus Ruwa'ichi, Bw. Bryan alisifu na kupongeza utashi wa Kisiasa na Uongozi wa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika kuhakikisha huduma za afya zinawafikia wananchi , ushirikiano wake na kutambua kwake mchango wa sekta binafsi katika eneo hilo.
Balozi Manongi na Upendo Manongi wakiwa na Padre Dkt. Peter Le Jacq wa Shirika la Maryknoll ambaye alianza kufanya kazi na Bugando Medical Center katika miaka ya 80 ambaye kwa kushirikiana kwa karibu na Marehemu Mhashamu Askofu Aloysius Balina walianza juhudi za kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya sekta ya afya hasa upungufu wa Madaktari. Padre Dkt. Jacq pamoja na rafiki zake alikuwa chumbuko la Kamati ya Touching Tanzania katika miaka hiyo ya 80 na hatimaye kuzaliwa kwa Touch Foundation mwaka 2004. Dkt. Jacq naye kwa upande wake amesifu na kutambua mchango wa Mhe. Rais Jakaya Kikwete na kujituma kwake kuimarisha sekta ya afya kwa kushirikiana na wadau wengine.
Makamu Mkuu wa CUHAS Professa Jacob Mtabaji kushoto kwa Balozi Manongi na Professa Paschalis Rugarabamu ambao walikuwa sehemu ya Ujumbe uliohudhuria Asante Supper 2014 wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maofisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2014

    Don show my identity nitafukuzwa chuo mroma si unamjua

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...