Bendi ya muziki wa dansi ya The African Stars ‘wana twanga pepeta’ ijumaa itazindua ukumbi wa kisasa wa burudani na mikutano wa Machinga Lounge uliopo maeneo ya uwanja wa mpira wa wa miguu wa Karume jijini.

Ukumbi huo unamilikiwa na kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET), umetengenezwa  kisasa zaidi kwa lengo la kuwapa burudani mashabiki wa Manispaa ya Ilala, Temeke na Kinondoni kwa mujibu wa mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka.

Asha alisema kuwa kwa muda mrefu sasa wakazi wa maeneo ya Ilala hawana ukumbi mkubwa kwa ajili ya shughuli za burudani na yeye kuamua kutengeneza ukumbi huo uliopo eneo maarufu la Machinga Complex.

“Hii ni fursa pekee kwa wadau wa burudani kuzindua ukumbi huo ambao ni wa kisasa, lengo ni kuwapa burudani mashabiki wetu wa maeneo hayo na majirani zake, hasa kwenye ukumbi wa kisasa ambao hata shuguli za mikutano mbali mbali inaweza kufanyika,” alisema Asha.

Alisema kuwa ukumbi huo unauwezo wa kuingiza watu zaidi ya 500 waliokaa kwenye viti na lengo lao kubwa pia kutumika kwa vikundi vingine vya burudani. “Twanga haitakuwa inafanya shoo zake mara kwa mara kwenye ukumbi huu, vikundi vingine, anamuziki wa bongo fleva na taarabu pia wanakaribishwa, kuutumia,” alisema.

Hii ni mara ya pili kwa ASET kumiliki ukumbi ambapo mwanzoni mwa miaka ya 2000 walimiliki ukumbi wa ASET Club (zamani FM Club au Lang’ata) uliopo eneo la Kinondoni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. mtoto wa mkulima juniorMay 07, 2014

    ankal tungepata mandhari ya ukumbi huo ili tuone tunachagua vitu gani vya ziada kwenye ukumbi huo mpya zaidi ya vile tunavyoviona kwenye kumbi tulizozoea kuzitembelea kila jumamosi, weekend au siku nyinginezo tunapokwenda kujivinjari.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 08, 2014

    Hongereni sana Twanga Pepeta kwa kufungua ukumbi wa burudani,nyinyi ni mfano wa kuigwa na tunaamini sana kweli mnaithamini na kuitlia maanani
    sanaa za maonyesho.
    WADAU
    Ngoma Africa Band aka FFU Ughaibuni,
    Ujerumani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...