Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, katika mkutano wake uliofanyika siku ya Alhamisi ambapo ilishindikana kupitisha Rasimu ya Azimio lililotaka kuipeleka Syria katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC) baada ya Urusi na China ambazo ni wajumbe wa kudumu wa Baraza hilo kupiga kura ya turufu (veto) huku nchi 13 zikipiga kura ya kuunga mkono.
Na Mwandishi Maalum
Siku chache baada ya Bw. Lakhdar Brahimi ,Mjumbe wa Maalum wa Katibu
Mkuu na Muungano wa Nchi za Kiarabu kujiuzulu na usulushi wa mgogo wa Syria.
Wananchi wa Syria wamepata pigo jingine, baada ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja
wa Mataifa, kushindwa kupitisha Azimio ambalo lingeipeleka Syria katika Mahakama
ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC).
Baraza Kuu la Usalama, lilikutana siku ya alhamisi ili kupigia kura rasimu ya Azimio
hilo lilowasilishwa na Ufaransa, lakini likashindwa kupita baada ya Urusi na Uchina
kupiga kura ya tururfu kupiga azimio hilo.
Wajumbe kumi na tatu kati ya 15 wanaounda Baraza hilo, walipiga kura ya kuunga
mkono rasimu hiyo.
Kama Azimio hilo lingepita bila ya kupingwa, basi ICC ingepewa dhamana ya
kuchunguza makosa yote ya jinai na uhalifu wa kivita kuanzia mwaka 2011 ulipoanza
mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe ambapo zaidi ya watu 100.000 wamepoteza
maisha huku mamilioni wakiwa ni wakimbizi.
Katibu Mkuu Ban ki Moon katika salamu zake zilizosomwa kwa niaba yake na Naibu
Wake Bw. Jan Eliason, muda mfupi kabla ya kupinga kura, amesema, Baraza Kuu
la Usalama na lile la haki za Binadamu yanawajibika kumaliza umwagaji damu na
kuhakikisha kwamba haki inatendeka kwa wahanga wa machafuko hayo.
Akaongeza kuwa wananchi wa Syria wanayo haki ya msingi ya kupata haki. Umoja
wa Mataifa na wananchama wake wanaowajibu wakuilinda haki hiyo. Kwa kuunga
mkono mifumo ambayo itawawajibisha wahalifu wa makosa ya kivita. Na kusisitiza
kwamba ni wazi kuwa hakuna upande wowote kati ya zinazopingana ambao hauna
kosa.
Akasisitiza kuwa kama wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama wataendelea kuto
kukubaliana kuhusu njia zinazoweza kuleta uwajibikaji juu ya uhalifu unaoendelea,
hadhi ya chombo hicho muhimu na Umoja wa Mataifa kwa ujumla itaendelea
kuathirika.
“ Tunapozungumzia uwajibikaji, lazima tufikirie si tu kwa pande zinazopingana, bali
pia ni lazima tuwafikirie na wale ambao wanaendelea kuchochea mgogoro huu na
kuendelea kwa madhara yanayotokana na wao kuendelea kutoa silaha kwa wale
wanaotenda uhalifu” akasema Ban ki Moon.
Akawasihi wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama, kuweka pembeni tofauti zao na
kufanya kazi pamoja ili kuumaliza mgogoro wa Syria pamoja na kutafuta suluhisho la
kisiasa.
Kabla ya kuwasilisha wa Azimio hilo mbele ya Baraza Kuu la Usalama, kulikuwa
na taarifa za kidiplomasia kuwa waandaji wa Azimio hilo walikuwa wakiziomba nchi
ambazo si wajumbe wa Baraza Kuu kuunga mkono hali ambayo si ya kawaida.
Well done Russian and China! Haya mataifa makubwa ya magharibi yanataka kutufanya sisi wote wajinga.
ReplyDeleteWao ndiyo waliowapa silaha wale waasi wa Syria. Na baada ya kuona kuwa walikuwa wanapeleka silaha kwa Al Qaida na kushindwa kumuondoa Assad wanapeleka Muswada kwenye Baraza la Usalama ili wapate walichokitaka kwa mlango wa nyuma.
Wamekuwa wanafanya hivyo hivyo Ukraine na kuindoa serikali halali ya Yanukovich, sasa wahuni wameingia madarakani kwa kuwa wapo upande wao basi wao ni halali na Yanukovich ni batili.
Wamefanya hivyo Libya na kinachoendelea wote tunakiona.
Inabidi wakutane na wanaume wenzao Mrusi na Mchina ndipo wanashika adabu.
Bahati mbaya sana siku hizi Propaganza za CNN na BBC zinakufanya ukosekupata haki ya habari katika maadili ya kiuandishi kama inavyostahili. Tumebakia kulishwa fikra zai ili tufikiri kama wao.
Nafikiri Dunia inahitaji ujasiri wa Mzee Mugabe na watu kama Putin na China ili kuwe na uwiano thabiti, na fikra huru.