Scott Eisner (kulia)vice President of African Affairs, US Chambers of Commerce akifungua sherehe ya uzinduzi wa kitabu cha wekeza Afrika 2014 iliyofanyika US Chambers of Commerce Washington, DC siku ya Jumatatu May 19, 2014 wengine katika meza ni Balozi wa kudumu wa African Union Mhe. Amina Salum Ali na Paul Duffen ambaye ni News Desk Media. 

Sherehe ya uzinduzi wa kitabu cha wekeza afrika 2014 ".invest in africa 2014" kitabu kinachotolewa na ubalozi wa umoja wa afrika ilifanyika Jumatatu May 19, 2014 kama kuanzia wiki ya kusherehekea siku ya afrika tarehe 27 mwezi mei .

Katika sherehe hizi zilizoandaliwa kwa pamoja baina ya ubalozi wa afrika washington na jumuia ya wafanya biashara wa marekani US chamber of commerce.

Kulikuwa na majadiliano yaliyofanywa na viongozi wanao wakilisha Mabalozi wa kanda 5 za afrika zikiwemo East.West .South Central na North.viongozi hao walizungumzia rasilmali zilizopo Afrika na kuwaalika wawekezaji wawekeze afrika kwani kuna faida kubwa zinapatikana. 


Kwa upande wa serikali ya marekani ilihudhuriwa na mwakilishi wa msaidizi katibu wa ofisi ya mambo ya nje ya marekani na mgeni mwengine wa heshima ni muwakilishi wa umoja wa matIfa united nation global compact.kitabu kilichotoka mwaka huu pia kimeelezea mafanikio yaliyopatikana afrika na muelekeo katika miaka ijayo.

 Sherehe ya uzinduzi wa kitabu cha wekeza Afrika 2014 ikiendelea.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...