![]() | |
Meneja uhusiano wa mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) Bw. Paschal Shelutete akizungumza wanahabari kuhusiana na tuzo za Uandishi wa Habari za Shirika la Hifadhi za Taifa za mwaka 2013. |
Jumla ya Waandishi wa Habari 10 wamefanikiwa kufikia hatua ya
fainali ya Tuzo za Uandishi wa Habari za
Shirika la Hifadhi za
Taifa za mwaka 2013.
Wanahabari waliofanikiwa kufika hatua ya
fainali ni
pamoja na Frank Leonard (Habari Leo), Jackson Kalindimya (Nipashe), Humphrey
Mgonja (Radio SAUT FM), Raymond Nyamwihula (Star TV) na Vedasto Msungu
(ITV).
Wengine
ni pamoja na Kakuru Msimu (Star TV), Gerald
Kitabu (The Guardian), Salome Kitomari (Nipashe), David Rwenyagira (Radio 5) na
Cassius Mdami (Channel Ten).
Hafla ya
utoaji Tuzo za Habari za TANAPA itafanyika
siku ya Jumanne tarehe 27 Mei, 2014 jijini Mwanza ambapo Mgeni Rasmi
anatarajiwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro
Nyalandu.
Hafla
hii itaenda pamoja na Mkutano wa kila mwaka
baina ya TANAPA na Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari
nchini inayotarajiwa kuanza wiki ijayo jijini Mwanza.
Jumla ya
kazi zilizotumwa kwa ajili ya
kushindanishwa mwaka huu ni 114 tofauti na kazi 34 za mwaka jana. Ongezeko hili
la asilimia 235 lililazimu Jopo la Majaji kutumia muda mwingi zaidi wa kupitia
kazi zote na kupata washindi. Kati ya kazi 114 zilizotumwa, kazi zilizohusu
Uhifadhi ni 64 (sawa na 56%) na kazi zilizohusu Utalii wa Ndani zilikuwa 50
(sawa na 44%).
Tuzo za
Uandishi wa Habari za TANAPA hutolewa kila
mwaka kwa nia ya kuwashirikisha wanahabari kushindanisha umahiri wa kazi zao
katika kuelimisha jamii umuhimu wa dhana ya Uhifadhi kwa maeneo yaliyotengwa
kisheria kama Hifadhi za Taifa na uhamasishaji wa Utalii wa Ndani kwa faida ya
uchumi wa nchi yetu.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
23.05.2014
Hifadhi za Taifa Tanzania
23.05.2014
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...