Mke wa Makamu wa Raisi Zakia Bilali akiwasha jiko la gesi ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mtambo wa gesi inayo tokana na kinyesi cha ng’ombe ambayo imetengenezwa na washiriki wa shindano la Maisha Plus kulia kwake ni mlezi wa chama cha wake wa viongozi New Mellinium Women Group Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda wakiwa na wake wengine wa viongozi wakishuhudia uzinduzi huo ambao umefanyika katika kambi ya Maisha Plus iliyopo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani
Mlezi wa chama cha wake wa viongozi New Mellinium Women Group Mama Tunu Pinda akiwongoza wakina mama wenzake kuelekea katika kambi ya Maisha Plus. Nyuma yake ni Mke wa Makamu wa Raisi Zakia Bilali. Wakina mama hao walifika katika kambi hiyo ili kujionea shughul zinazo fanywa na washiriki katika maisha Plus iliyopo Bagamoyo Pwani
Mke wa Makamu wa Raisi Zakia Bilali akiwa na Mlezi wa chama cha wake wa viongozi New Mellinium Women Group Mama Tunu Pinda pamoja na Katibu wa chama hicho cha wake wa viongozi Mama Pamela Mathayo wakiangalia shamba la mfano ambalo washiriki wa maisha Plus wanaliandaa
Wanachama wa cha Wake wa Viongozi New Mellinium Women Group wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Maisha Plus wa hapa nchini na nnje ya nchi pamoja nawaandaji. Picha na Chris Mfinanga
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...