WANAHABARI mkoa wa Wa Lindi wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bw Abdulaziz Ahmeid wameadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kwa
kutoa msaada kwa jamiii baada ya kutoa msaada wa Vifaa mbalimbali
katika wodi za wazazi na watoto katika Hospital ya Rufaa ya Sokoine
Mkoani Lindi
Wanahabari hapo pia walipimwa afya zao na Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya mkoani humo ili kila mmoja afanye kazi zake huku akijua Afya
yake
Akiongea baada ya hafla hizo Bw. Abdulaziz Ahmeid alieleza kuwa katika maadhimisho
hayo ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Arusha ambayo yana kauli mbiu
ya Uhuru wa Habari kwa maendeleo na utawala bora Ambapo wanahabari
wameamua kurudi kwa jamii kwa kuona umuhimu wa kusaidia
wagonjwa,Wazee na Walemavu
"Ni Vyema waandishi tukajenga Utayari wa kusaidia Jamii na ndizo zenye
Uhitaji wa misaada muhimu na hata kihabari kuliko kujikita na
wanasiasa kwa maslahi yao na wakati wao tu Muhimu Tujitambue tutetee
haki zetu ikiwemo Kuajiriwa na kufungwa kwa mikataba kuliko ilivyo
sasa zaidi ya asilimia 90 HATUJIELEWI.
"Sambamba na hilo Tujikite katika kuandika habari za Uchunguzi na fursa
zipo kupitia TMF..Alimalizia Abdulaziz.
Nae Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Lindi Bi
Fortunata Kullaya ambae alikuwa Mgeni Rasmi katika sherehe hizo
zilizokutanisha waandishi toka wilaya zote za mkoa wa Lindi aliwataka
Waandishi kuandika habari kwa kufuata maadili ili wasijiingize katika
matatizo hasa katika kipindi hiki cha mchakato wa katiba na kuelekea
katika uchaguzi mkuu hapo mwakani kwa kuwa wanahabari ni watu muhimu
katika jamii.
Pia aliwataka kufika vijijini kubaini baadhi ya
changamoto ambapo pia aliwahakikishia kuwa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF
sasa ndio mkombozi wa huduma za afya hivyo pelekeni Ujumbe Jamii
Ijiunge na ipate Tiba kwa Unafuu zaidi
Nyie ni wadau wakubwa wa NHIF, hivyo mbaini kuwa kalamu zenu zinaweza
kujenga au kubomoa hivyo bima ya afya Tawi Lindi
"Tumeona ni siku
muhimu sana kujumuika pamoja kwa kuwapima afya zenu ili mfanye kazi
mkijijua
Aidha katika maadhimisho hayo pamoja na lutoa msaada kwa Wagonjwa wa
hospital ya Rufaa ya Sokoine na kupimwa kwa Afya za Waandishi
hayo yalifuatiwa na Tafrija Fupi ya Kutakiana heri iliyojumuisha waandishi na
Wenza wao pamoja na wadau wengine wa habari iliyofanyika katika Fukwe
za Santorin Beach Manispaa ya Lindi
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa Habari Lindi Bw. Abdulaziz Ahmeid akipimwa afya yake na daktari wa NHIF Timoth Mwasajone katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari
Picha ya pamoja ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Mfuko wa NHIF Mara baada ya mfuko huo kujitolea kupima Afya za waandishi wa Lindi
Mwandishi wa Tbc Lindi Martina Ngulumbi akimbeba mtoto toka kwa mama alietoka kujifungua siku ya uhuru wa habari
.Mwenyekiti wa LPC ,Abdulaziz Ahmeid akikabidhi msaada Kwa Muuguzi wa zamu Bi Habiba Chitanda msaada uliotolewa na Wanahabari wa Lindi
Mwenyekiti Abdulaziz akisalimia baadhi ya watoto waliolazwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya Sokoine mjini Lindi mara baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali katika kusaidia jamii katika siku ya uhuru wa habari
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...