WATANZANIA wametakiwa kujenga utamaduni wa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kabla ya kuugua ili kuepukana na usumbufu mkubwa ambao umekuwa ukijitokeza.

Rai hiyo imetolewa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Ilala Bw. Christopher Mapunda wakati akiwasilisha mada katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.

Amesema kuwa utafiti unaonesha watu wengi huanza harakati za kutaka kuwa na bima ya afya wakiwa na wagonjwa na wanapoona gharama za matibabu zinawalemea.

“Watu wengi wanaanza harakati za kutafuta namna ya kujiunga na Mfuko wakati wana wagonjwa wako hospitali na hii inasababisha usumbufu mkubwa na wakati mwingine kuuona Mfuko una urasimu..ni vyema tukawa na utamaduni sasa wa kujiunga kabla ya kuugua,” amesema Mapunda.

“Utaratibu wa kujiunga na Mfuko utasaidia sana kupunguza gharama za matibabu kwa walengwa lakini pia kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya mijini na vijijini,” amesema.

Aidha Mapunda alitumia mwanya huo kuwataka watumishi ambao hawajajaza fomu za Mfuko kuzijaza ili waweze kupata vitambulisho vya matibabu kwa wakati lakini pia wazitumie Ofisi za Mfuko ambazo ziko katika mikoa mbalimbali kupata ufafanuzi au kutatua kero walizonazo.

Kwa upande wa waajiri, aliwataka kuwasilisha michango kwa wakati na kuambatanisha nakala ya wachangiaji ili kurahisisha uhakiki wa michangoya kila mwezi.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Ilala Christopher Mapunda akiwasilisha mada kwa washiriki wa mafunzo kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
 Sehemu ya washiriki kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima wakifuatilia mada ya umuhimu wa kutumia huduma za NHIF.
 Washiriki wakifuatilia mada kwa makini zaidi.
 Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada.
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Meneja wa NHIF Mkoa wa Ilala

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...