Mkuu wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania, Brigita Stephen(katikati)akitangaza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuanza kutumika kwa mfumo mpya wa usajili wa nambari za wateja wa kielektroniki jijini Dar es salaam. kushoto ni Ofisa Mkuu wa huduma kwa wateja Harriet Lwakatare na Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliana Kwa wa kampuni hiyo Rosalynn Mworia. Tofauti na utaratibu wa kawaida wa usajili unaotumia zaidi ya siku kumi na tano, mfumo huo unakamilisha zoezi la usajili ndani ya saa moja kutoka mahali popote mteja alipo.
Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia(kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)wakati wa kutangaza matumiiz ya mfumo mpya w akielektroniki wa usajili nambari za wateja kupitia simu za mkononi. Kutoka kushoto ni Ofisa Mkuu wa huduma kwa wateja Harriet Lwakatare na Mkuu wa Idara ya huduma kwa wateja wa kampuni hiyo Brigita Stephen. Tofauti na utaratibu wa kawaida w ausajili unaotumia zaidi ya siku kumi na tano, mfumo huo unakamilisha zoezi la usajili ndani ya saa moja kutoka mahali popote mteja alipo.
Mkuu wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania, Brigita Stephen akiwaonesha waandishi wa habari usajili wa wateja kwa njia ya kielektroniki kupitia simu za mkononi ulioanza kutumiwa na Vodacom ili kurahisisha kazi ya usajili. Tofauti na utaratibu wa kawaida wa usajili unaotumia zaidi ya siku kumi na tano, mfumo huo unakamilisha zoezi la usajili ndani ya saa moja kutoka mahali popote mteja alipo.
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania inawawezesha wateja wake kufanya usajili wa nambari zao za simu kwa njia ya kielektronikia kupitia simu za mkononi, mfumo ambao unatoa urahisi kwa kila mteja kukamilisha zoezi la usajili ndani ya muda mfupi zaidi wa chini ya saa moja.
Kusajili kwa kutumia njia za kawaida, zoezi la usajili huweza kutumia hadi siku kumi na tano kutoka siku mteja alipojaza fomu ili kutoa nafasi kwa wakala aliyesajili kutuma fomu jijini Dar es salaam kwa uhakiki na uthibitisho wa taarifa za msajiliwa.
Mfumo huo wa kielektroniki, mchakato wote wa usajili hukamilishwa kwa njia ya simu ya mkononi kwa kuwa humpa uwezo wakala wa Vodacom kupiga picha kitambulisho cha mteja, kuhakikia taarifa zake na hivyo kuzituma moja kwa moja tayari kwa hatua ya mwisho ya usajili. Kw akutumia TILL maalum.
Mfumo huo mpya wa usajili wa kielektroniki unakuja wakati ambapo wateja wetu wamekuwa wakitoa ushirikiano katika utekelezaji wa matakwa ya sheria ya huduma za Kielektroniki za Posta na Mawasiliano - EPOCA inayowataka watumiaji wa simu za mkononi nchini kutotumia laini ya simu isiyosajiliwa.
Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa Vodacom Brigita Stephen amesema "Tumekuwa na mafanikio makubwa katika usajili wa nambari za wateja wetu, tunawashukuru sana kwa ushirikiano wanaotupatia katika kutimiza matakwa ya kisheria."
Brigita aliongeza kwa kusema "Mfumo huu wa kielektroniki ni katika juhudi za kuwa na njia mbalimbali kuwawezesha wateja wetu kutojisikia shida katika kusajili nambari zao (SIM),hii ni matokeo ya nia ya wakati wote ya Vodacom kuhakikisha inaendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria, taratibu na kununi zinazosimamia sekta ya mawasiliano na nchi kwa ujumla.
Amesema SIM zote za Vodacom zinazouzwa sokoni huwa haziwezi kuwa hewani kwa matumizi yoyote hadi pale mteja anapokamilisha zoezi la usajili ikiwemo wa awali wakati usajili kamili unapofanyiwa kazi na kinyume cha hapo Vodacom huifungia SIM husika.
Vodacom inaendelea kuwakumbusha mawakala wake wa mauzo ya SIM kuendelea kuwakumbusha wateja umuhimu wa kusajili nambari zao sio tu kwa usalama wao bali pia kuweza kutambulika na kupata msaada kutoka Vodacom pale wanapopatwa na tatizo ikiwemo kwenye huduma za M-pesa, kupoteza simu n.k.
Mwaka jana wakati wa zoezi la utekelezaji mpango wa usajili wa nambari za simu chini ya maelekezo ya Mamalaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Vodacom ilizifungia SIM zaidi ya laki nne baada ya kutokuwa zimesajiliwa mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha mpito.
Chini ya Sheria ya EPOCA mteja anaetumia laini ya simu ya mkononi isiyosajiliwa kisheria hutiwa hatiani na hupaswa kulipa faini ya Shilingi 300,000 au na kifungo cha muda usiopoungua miezi sita gerezani au vyote kwa pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...