Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Blantyre nchini Malawi kwa ajili ya kushiriki mazishi ya aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Marehemu Flossie Gomile-Chidyaonga aliyefarikii dunia tarehe 09 mei, 2014 Jijini na Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa tarehe 14 Mei, 2014. Mhe. Membe anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye mazishi hayo. 
Balozi wa Tanzania nchini Malawi,  Mhe. Patrick Tsere akimweleza jambo Mhe. Membe wakati wa mapokezi.
Mhe. Membe akijaribu kumwelezea Rais wa Malawi, Mhe. Joyce Banda namna alivyozipokea taarifa za kifo cha Balozi Flossie. Kushoto kwa Mhe. Rais Banda ni mume wake Jaji Mkuu Mstaafu Banda na kulia kwa Mhe. Membe ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mhe. Ephraim Chiume.
Baadhi ya Wananchi wa Blantyre na sehemu nyingine za Malawi wakiwa uwanjani hapo wakati wa mapokezi ya Mwili wa aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Marehemu Flossie Gomile-Chidyaonga.
Mhe. rais Banda akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule. Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 15, 2014

    Bonge la bao tumempiga bibie isis tungali na ndege ya Raisi kama kawauda na maandishi makubwaaa TANZANIA!

    Raisi Joyce Banda akauza ndege ya Uraisi baada ya kuingia Ikulu mwaka 2012 akisaka Mtaji wa Kisiasa.

    Hivi jamani, baadhi ya vitu ni vya ajabu.

    Kuna tatizo gani Raisi wa nchi akitumia ndege Kikazi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...