Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Samuel Sitta anatarajia
kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara kwa
mwaka wa Fedha 2014/2015 kesho tarehe 22 Mei, 2014, ambapo atazungumzia
utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2013/2014 na makadirio ya
mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Hotuba
hiyo itapatikana kwenye tovuti ya Wizara www.meac.go.tz na
kwenye vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya Mhe. Waziri kumaliza kuisoma
Bungeni.
Tunawakaribisha
wadau mbalimbali wa masuala ya Mtangamano wa Afrika Mashariki na wananchi kwa
ujumla kufuatilia kwa karibu hotuba hiyo ili kuongeza uelewa wa masuala ya
Matangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Imetolewa
na:
Katibu Mkuu
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki
+255 222126827, 2126830
+255 713341354
Email:
ps@meac.go.tz
Website:
www.meac.go.tz
21
Mei, 2014
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...