Katika hali ya kushangaza na kusikitisha, wezi wasiofahamika wameiba baadhi ya miundombinu ya soko la Ngiu wilayani Makete mkoani Njombe licha ya soko hilo kuwa na mlinzi.
Mwandishi wa blog hii ambaye amefika eneo la tukio mara baada ya kupenyezewa taarifa hizi na wananchi, ameshuhudia baadhi ya miundombinu haipo ikiwemo mifuniko yote ya chuma inayofunikia masinki ya vyoo, pamoja na mabomba ya kutiririshia maji ya mvua
Taarifa kamili na picha zote za tukio hilo zitakujia baadaye kidogo.
Muonekano wa soko la Ngiu lililopo kata ya Iwawa, Makete mjini.
Chemba ya choo cha soko hilo ikionekana baada ya wezi kuiba mifuniko yote mitatu ya kufunikia chemba hiyo
Na Edwin Moshi wa globu ya jamii, Makete
Dah....huzuni kubwa hii.....yaani nadhani hata ndala, fulana, sketi bado dili huko nyumbani yaani ukijipindua watu wanaramba....huu ni wehu...utaibaje vitu vya umma?? japo wengine nao wanahomola...kama ripoti za mahesabu zinavyotujuza.....ni huzuni kubwaaaa.....
ReplyDeleteWenye kushughulikia vyuma chakavu waangaliwe. Muweke mifuniko ya chemba ya smenti mkirudisha ya vyuma wataitoa.
ReplyDelete