Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi akiongea na wadau mbalimbali wa elimu wa mkoa wa Dar es salaam wakiwemo walimu wa shule za msingi na sekondari,wamiliki wa shule binafsi na wanafunzi wakati wa hafla ya Siku ya Elimu mkoani Dar es salaam leo.Katika hafla hiyo washindi wa mitihani ya taifa kwa mwaka 2013 kutoka shule za msingi na sekondari za serikali na binafsi wametunukiwa vyeti na zawadi mbalimbali kutokana na ufanisi wao katika utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
 Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Raymond Mapunda akiongea na wadau mbalimbali wa elimu wa mkoa wa Dar es salaam wakiwemo walimu wa shule za msingi na sekondari,wamiliki wa shule binafsi na wanafunzi wakati wa hafla ya Siku ya Elimu mkoani Dar es salaam.
 Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za jijini Dar es salaam waliohudhuria hafla ya Siku ya Elimu mkoa wa Dar Es Salaam wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea wakati wa hafla hiyo.
 Wadau wa elimu wakiwemo wazazi, walimu wa shule za sekondari na msingi, wamiliki wa shule binafsi na viongozi mbalimbali wakishangilia mafanikio na ushindi wa mkoa wa Dar es salaam katika mitihani ya taifa ya shule za Msingi na Sekondari  kwa mwaka 2013 leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya Siku ya Elimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...