Na Woinde Shizza, Arusha
Jaji mstaafu Mark Bomani leo amezindua rasmi video ya wimbo
wa waandishi wa habari ujulikanayo kwa jina la Uhuru wangu pamoja na
albamu mpya ya msanii wa mziki wa nyimbo za asili Mrisho Mpoto
ijulikanayo kwa jina la Waite katika kilele cha maathimisho ya uhuru
wa vyombo vya habari duniani jijini Arusha.
Uhuru wangu uko wapi mwanahabari mie,kalamu yangu,sauti yangu kamera
yangu leo ndio kaburi langu mie
Huo ndio wimbo wa kundi la Mrisho Mpoto Band ambalo ulikuwa
ukiwaburudisha wanahabari katika uzinduzi wa albamu Mrisho Mpoto
Band,unaoelezea mambo mbalimbali wanayokumbana nayo wanahabari wa
vyombo mbalimbali vya habari.
Akighani mashairi ya wimbo huo katika uzinduzialisema poleni sana misa
Tanzania,TMF,MOAT,UTPC ,TCRA kama mtu ile timu ya watu watano
tuyioituma Ujerumani ,Norway,Sweden ipo wapi ripoti yake
kiongea wakati wa uzinduzi wa albamu hiyo pamoja na wimbo huo wa
wanahabari msanii mrisho mpoto alisema kuwa yeye alifarijika sana pale
alivyofatwa na wanahabari na kumuomba awatungie wimbo ambao
unawahusu wanahabari pamoja mambo ambayo yanawakabili.
Alisema kuwa wamekaa wakashauriana na timu yake na bendi yake kuwa
watu wasanii wengi wamekuwa wakizindua albamu kwa kuweka viingilio
vikubwa kualika watu wengi lakini yeye binafsi ameamua kuzindua albamu
hii katika siku hii ya waandishi wa habari kwa kuwa wamemtoa mbali na
ana kitu cha kuwapa zaidi ya kuwapa zawadi hii ya kuzindua albamu
yake mbele yao.
Alibainisha kuwa mbali nakuzindua albamu hiyo pia kwa kuwa waandishi
wamempa hadhi ya kuwatungia wimbo pia anajitolea kuweka wimbo huu wa
waandishi wa habari ndani ya albamu yake ili kila mtanzania na
mshabiki wake ambaye atanunua albamu yake aukute wimbo ndani ya
albamu yake.
"Hii albamu yangu itakuwa na nyimbo zangu zote ikiwa na wimbo wa
nikipata nauli adi nyimbo zake zote ambazo zinajulikana na kiukweli
najisikia kulia sana kupewa heshima hii nzito ya kuzindua albamu yangu
na ata jana nilivyokuwa nakuja uku nilikuwa na zunguma na mh bomani
kuwa hii kwangu itakuwa ni historia katika maisha yake"alisema mpoto
Katika wakati wimbo huu ukiendelea wanahabari walionekana wakitoa
machozi kwa kuuzunishwa na tenzi zilizopo katika wimbo huu kwani
msanii huu ameuimba kiualisiazaidi.
Jaji mstaafu Mark Bomani akiongea wakati wa kuzindua rasmi video ya wimbo wa waandishi wa habari ujulikanayo kwa jina la Uhuru wangu pamoja na albamu mpya ya msanii wa mziki wa nyimbo za asili Mrisho Mpoto ijulikanayo kwa jina la Waite katika kilele cha maathimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani jijini Arusha.
Jaji mstaafu Mark Bomani akizindua rasmi video ya wimbo wa waandishi wa habari ujulikanayo kwa jina la Uhuru wangu pamoja na albamu mpya ya msanii wa mziki wa nyimbo za asili Mrisho Mpoto ijulikanayo kwa jina la Waite katika kilele cha maathimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani jijini Arusha. Chini Mrisho Mpoto akielezea wimbo wake.
Picha na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii, Arusha
Video na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...