Waziri wa Mambo ya Ndani yaNchi, Mathias Chikawe akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo katika Kikao cha Pili cha Baraza hilo kilichofanyika Giraffe Hotel jijini Dar es Salaam leo. Katika kikao hicho, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imependekeza kutumia Shilingi Bilioni 955.934 katika Mwaka wa Fedha 2014/2015. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi, Waziri wa wizara hiyo, Mathias Chikawe (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya kufungua mkutano wa wafanyakazi wa siku moja unaofanyika katika Hoteli ya Giraffe jijini Dar es Salaam. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia), Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (wapili kushoto), Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (kulia) na Katibu Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo, JenithaNdone wakiimba nyimbo ya mshikamo daima katika Kikao cha Baraza la Wfanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika katika Hoteli ya Giraffe jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akimkabidhi Staford Busumbiro (kushoto) Shiingi milioni Mbili kwa niaba ya Haidhuru Kita kwa kuchaguliwa kuwa mfanyakazi bora wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika mwaka 2014. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi na Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu, Mbarak Abdulwakil na Jenitha Ndone, Katibu Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2014/15 kwa Wajumbe wa wizara hiyo katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika katika Hoteli ya Giraffe, jijini Dar es Salaam. Katika Mwaka wa Fedha wa 2014/2015 wizara hiyo inatarajia kutumia Shilingi Bilioni 955.934. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watatu kulia-waliokaa). Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kushoto waliokaa), Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi (wapili kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa idara wa wizara hiyo na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kufunguliwa Kikao cha siku moja cha Baraza hilo kilichofanyika katika Hoteli ya Giraffe, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2014

    swali dogo naomba michuzi usinibanie

    hivi hii tabia ya kupeleka mikutano kwenye hoteli binafsi itaisha lini? wizara ya mambo ya ndani hapo kati kati ya jiji ina jengo jipya ambalo nina uhakika haliwezi kosa ukumbi wa mikutano wa kuweka hicho kikao ... kwa nini waingie gharama kwenda kukodi ukumbi mwingine, gharama na muda wa kusafiri kwenda kwenye huo ukumbi mwingine

    kuweni na huruma na hela za walipa kodi wa tanzania ... kuna watu wanakufa kwa kukosa dawa na huduma nyingine ndogo ndogo huku watu wachache waliopata neema za kuajiriwa na kusimamia shughuli mbali mbali za serikali wanachezea hela kama hivi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...