Wauguzi wa Zanzibar wakila kiapo cha Utii katika maadhisho ya siku ya wauguzi Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 12 Mei. Maadhimisho hayo yalifanyika Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongochekundu
Wauguzi wa Zanzibar wakiimba nyimbo ya siku ya wauguzi Duniani katika maadhimisho yaliyofanyika Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongochekundu.
Muuguzi Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Bi. Wanu Bakari Khamis akisoma risala ya siku ya wauguzi Duniani katika maadhimisho yaliyofanyika Kidongochekundu.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jidawi akimkabidhi zawadi Muuguzi Ramla Kombo wa Kituo cha Afya Unguja Ukuu kwa kuwa miongoni mwa wauguzi waliofanya vizuri zaidi mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yaliyofanyika Kidongochekundu.
Muuguzi Rajab Khamis Rajab akipokea zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya ya Zanzibar kwa kuwa miongoni mwa wauguzi waliotekeleza wajibu wao kwa ufanisi zaidi mwaka huu.
Wauguzi wa Zanzibar wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk. Muhammed Jidawi (hayupo pichani) katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yaliyfanyika Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongochekundu. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...