Majeruhi akipewa huduma ya kwanza na mmoja wa akina mama aliyekuwa akifanya usafi kando kando ya barabara mapema leo asubuhi,katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha.
Baadhi
ya Watu wakitazama ajali ya magari mawili kama yaonekanavyo
pichani,iliyotokea mapema leo asubuhi eneo la Moroco-Posta jijini
Dar,katika ajali hiyo ambayo chanzo chake hakikufahamika mara moja,mtu
mmoja alijeruhiwa na kukimbizwa hospitali kwa huduma ya kwanza,hakuna aliyepoteza maisha.
Mama
ambaye jina lake halikufahamika mara moja moja aliyekuwa kwenye gari
lenye usajili wa namba T679 CKC,akipewa huduma ya kwanza mara baada ya
kupoteza fahamu
Moja ya gari ambalo pia lilipata ajali mara baada ya kuacha barabara na kuvamia mtaro kama lionekanavyo pichani.
Moja
ya gari ambalo pia lilipata ajali mara baada ya kuacha barabara na
kuvamia mtaro kama lionekanavyo pichani,huku abiria wake mmoja akiwa
amepoteza fahamu,kama aonekavyo kwa mbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...