Balozi Modest Mero na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Bi. Agness Kijazi katika picha ya pamoja, kwenye makazi ya balozi Tanzania nchini Geneva
Hivi karibuni Mh. Modest Mero, Balozi wa Tanzania, Geneva alifanya
mazungumzo ya pamoja na Mh. Dkt. Seif Rashid na Bi. Agness Kijazi,
katika makazi ya Balozi, Geneva.
Ujumbe wa Mh.
Waziri ulikuwa Geneva kwenye kikao cha Bodi ya " Global Alliance for
Vaccines and Immunization", Geneva, ambapo Mh. Waziri ni mjumbe wa Bodi.
Na pia ujumbe wa Mkurugenzi wa Hali ya Hewa upo Geneva kuhudhulia kikao
cha 60 cha kamati kuu ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (World
Meteorological Organization).
Mh. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii katika mazungumzo na Balozi Mero, kwenye makazi ya balozi, Geneva, Uswisi.
Wakijiandaa kupata mlo wa pamoja baaada ya mazungumzo
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh.Dkt. Seif Rashid, Balozi Mh. Modest Mero na Mrs. Rose Mero na msaidizi wa Waziri katika picha ya pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...