Balozi Seif akizungumza na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Kijiji
cha Kiboje Mamboleo mara baada kuufungua msikiti wao wa Ijumaa uliofanyiwa
matengenezo makubwa.Picha na
Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Moh’d Raza Hassanali akielezea
mikakati ya kamati ya ujenzi wa misikiti, Madrasa na maskuli nchini ilivyopania
kuendeleza malengo yake.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amezikumbusha Kamati za Misikiti
hapa nchini kuendelea kuwa imara kwa
kutowaruhusu watu wanaopenda kujipenyeza ndani ya kamati hizo kwa nia ya kuanza
kutoa madarasa ya uchochezi na kuwagawa waumini kimadhehebu.
Alisema
uimara huo ndio njia sahihi itakayoilinda misikiti hiyo na wimbi la vurugu na
migogoro ambayo hatiae husababisha mmong’onyoko mkubwa wa ukosefu wa maadili katika jamii za kiislamu.
Akiufungua
msikiti mpya wa Ijumaa uliofanyiwa matengenezo makubwa katika Kijiji cha Kiboje
Mambo leo Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif alisema msikiti ni taasisi yenye mchango mkubwa wa
kuutangaza ukweli dhidi ya unafiki pamoja na mambo ya kheri kwa jamii ya
Kiislamu.
Balozi Seif
alisema katika kuihuisha nyumba ya Mwenyezi Muungu Msikiti ni vyema kwa waumini hao mbali ya
kutekeleza vipindi vya sala lakini pia ni vyema wakaendeleza madarasa hasa
kipindi hichi kinachokaribia cha mfungo
wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kujifunza masuala ya dini yao.
Akisoma
risala ya waumini na wananchi hao wa Kiboje Mamboleo Ustadhi Juma Abdulla
alisema wana jamii hao wameelezea faraja yao kutokana na kumalizika kwa ujenzi
wa msikiti huo,lakini hata hivyo bado zipo baadhi ya changa moto zinazoendelea
kuwakabili wana jamii hao wa Kiboje Mambo leo ambazo zimekuwa zikiwapa wakati
mgumu kwao na kizazi chao.
Mapema
Mwenyekiti wa Kamati ya usimamizi wa ujenzi wa Misikiti, madrasa na majengo ya
skuli hapa Zanzibar ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Moh’d Raza
Hassanali alisema kamati hiyo iliyo chini ya mwenyekiti wake Rais Mstaafu wa
Tanzania Alhajj Ali Hassan Mwinyi itaendelea kuongeza nguvu zake kwenye ujenzi
wa majengo ya taasisi hizo yenye upungufu hapa Nchini.
Othman
Khamis Ame
Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
27/6/2014.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...