Na Mwandishi Wetu

Benki ya CRDB imetoa misaada mbalimbali kwa watoto wasiojiweza katika kituo cha Msimbazi centre.

Hatua hiyo imetokana na maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yenye kauli mbiu ya elimu bora kwa wote.

Akizungumza Jana jijini Dar es salaam Meneja wa benki hiyo Tawi la Premier, Fabiola Mussula, alisema kuwa benki hiyo imeadhimisha siku ya mtoto  wa Afrika kwa kupitia akaunti ya Junior Jumbo.

Alisema kuwa akaunti ya mtoto  humsaidia mzazi kuhakikisha anahifadhi ada na kulipa kwa wakati pindi inapotakiwa.

Fabiola alisema kuwa ni vyema wazazi wa kitanzania wakaweka akiba ya mtoto  ili kupunguza ukali wa maisha unaowakuta wazazi wengi.

" akaunti hii itambana mzazi kutokutoa hela Mara kwa Mara, na itamruhusu katika msimu wa ada pekee lakini pia anaweza akatuambia sisi watu wa Benki na tukamlipia shuleni na ni akaunti isiyo na makato"alisema.

Naye Neema Tarimo, alisema yeye kama mzazi Hutumia akaunti ya mtoto  kwa kuhifadhi ada za watoto wake na kuongeza kuwa humsaidia kumbana kutotoa fedha kila wakati na badala yake huzitoa pindi anapohitaji ada.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Premier, Fabiola Mussula akizungumza waandishi wa habari kuhusiana na Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika waliyoandaa kupitia akaunti ya Junior Jumbo kwa ajili ya watoto.
 Kila aina ya michezo ilikuwepo katika kuipamba Siku ya Mtoto wa Afrika. 
 Watoto wakicheza michezo mbalimbali nje ya Benki ya CRDB Tawi la Premier, uongozi wa Benki ya CRDB iliwaandali michezo mbalimbali watoto ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Meneja wa Akaunti ya Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Mary Kimasa akimlisha keki mmoja wa watoto wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Tawi la Premier  jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...