kufanikiwa kunyakuwa ubingwa huo. Wa pili kushoto ni bondia Shomari Milundi, kulia ni Promota aliyefanikisha safari hiyo Yaj Msangi, wadau Bilali Ngonyani na Rogers Masamu
-----------------------------
Bondia Mtanzania anaeshika rekodi namba moja nchini Ibrahimu Class 'King Class Mawe' amerudi na ubingwa wa WPBF nchini akitokeza Zambia ambapo alifanikiwa kumpiga kwa K,O mbaya sana bondia Mwansa Kabinga wa Zambia mchezo uliochezwa Arthur Davis Stadium, Kitwe, Zambia
Akizungumzia safari yake ya kuelekea kunyakuwa ubingwa huo alisema amepata tabu sana wakiwa njiani ambapo wame ondoka alhamisi usiku sana na kufika Jumamosi asubuhi nchini Kenya ambapo alizuiwa kutokana na kuwa na passport ndogo hivyo hakufanikiwa kwenda Zambia. Hapo Nairobi wakasaidiwa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, hat hivyo ndege waliyokuwa wapande ilikuwa imeshaondoka zamani
Baada ya hapo kuna pesa walitakiwa waongeze, wakaongeza kiasi kwa kudunduliza ndipo wakasafiri mpaka Zambia.
Huo ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza kucheza nje ya nchi tangia ajiunge na ngumi za kulipwa na kufanikiwa kunyakuwa ubingwa huo ambao umemuweka katika ramani nyingine kabisa ya kimataifa.
Bondia huyo alishukuru kwa kupokelewa naMkuu wa wilaya ya Kibondo Venance Mwamoto aliyekuja kwa niaba ya Serikali na kuahidi kumpatia mmoja ya michezo Kibondo au nchi jirani kwa ajili ya kumtangaza zaidi na kuendeleza kipaji chake hicho
Mkuu huyo wa Wilaya alisema "Watu wengi wanapenda mchezo wa ngumi hivyo kwa niaba ya serikali nitafanya jitiada nikupatie mchezo mmoja kwa ajili ya kutetea mkanda wako hata burundi ili uzidi kufahamika na kukuza kipaji chako"
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' hajawa nyuma kuwashukuru makocha wake ambao wamemwezesha kufika hapo ambao ni pamoja na Habibu Kinyogoli 'Masta', Kondo Nassoro, Sako Mtulya na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anamtafutia mapambano mbalimbali na humpa ushauri. 
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...