MUIGIZAJI MKONGWE HAPA NCHINI, SAID WA NGAMBA MAARUFU KWA JINA LA MZEE SMALL AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI ALIKOKUWA AMELAZWA AKIPATIWA MATIBABU YA KIHARUSI. ALIKUWA NA MIAKA 59.
AKITHIBITISHA TAARIFA YA KIFO CHA MZEE SMALL, MWANAE AITWAE MAHMOUD AMESEMA MZEE WAKE AMEFIKWA NA MAUTI HAYO MAJIRA YA SAA NNE USIKU WAKATI AKIWA HOSPITALINI HAPO AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU.
MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA NYUMBANI KWAO TABATA AMBAPO MAZISHI YANATARAJIWA KUWA KESHO SAA KUMI ALASIRI KATIKA MAKABURI YA TABARA SEGEREA JIJINI DAR ES SALAAM.
MZEE SMALL ATAKUMBUKWA KAMA MMOJA WA WACHEKESHAJI MAHILI KUTOKEA HAPA NCHINI, MARA KWA MARA AKIWA NA "MKEWE" WA JUKWAANI BI. CHAU.
MAISHA YA SANAA YA MZEE SMALL YALIANZIA KATIKA NGOMA ZA UTAMADUNI, AKIWA MMOJA WA WASANII WALIOKIWEZESHA KIKUNDI CHA MAGEREZA KUTAMBA SANA TANGIA MIAKA YA 1970 NA 1980.
ALIENDELEA KUWA NYOTA WA UTAMADUNI HATA BAADAYE ALIPOSTAAFU MAGEREZA NA KUJIUNGA NA KIKUNDI CHA RELI "KIBOKO YAO" NA BAADAYE NASACO, KABLA YA KUANZISHA KUNDI LAKE MWENYEWE NA HATIMAYE KUJITOSA KWENYE FILAMU, AKIWA MUIGIZAJI WA KWANZA KUCHEZA KOMEDI KWENYE TV.

GLOBU YA JAMII IMEPOKEA TAARIFA HII KWA MASIKITIKO MAKUBWA SANA NA INAMUOMBEA KWA MWENYEZIMUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI.
-AMIN.
Innalilahi wa innailayhi rajiuun.
ReplyDeleteRIP MZEE SMALL
ReplyDeleteInnaa liLlaahi wa innaa ilayHi raajiuwn.
ReplyDeleteinna lillah wa inna ilayhi rajiun
ReplyDeleteR. I.P
ReplyDeleteSooo sad, huyu bwana alikuwa na kipaji...RIP
ReplyDeleteRIP Mzee Small. Asante kwa kutuburudisha.
ReplyDeleteR.I.P Mzee wetu
ReplyDeleteNakuja haina hatakayedumu milele nasi tupo foleni.
ReplyDeletePumzika kwa amani MZEE wetu
INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUUN. Mwenyeez Mungu akughufirie kwa yote, akupumzishe pema unapostahiki na kesho uwe miongoni mwa waja wake wema katika yake Jannatu N'naeem.
ReplyDeleteKwa kweli kila nlipokuwa naiona hii kofia ya 'Tarbush' popote pale, cha kwanza hupata picha ya Mzee Small, gwiji wa vichekesho Tanzanzania. Rest In Peace Marehemu mzee wetu Bw. Said Ngamba almaaruf 'Mzee Small'.