![]() |
Kamishna wa Polisi Issaya Mngulu, Mkurugenzi wa
upelelezi wa makosa ya jinai nchini (DCI), akiongea na wanahabari mkoani Tabora Leo
|
ya Jamii, Tabora
MKUU wa Jeshi la Polisi hapa nchini IGP Ernest Mangu ameteua timu ya
askari polisi wataochunguza tuhuma za wizi wa fedha za wakulima wa zao
la tumbaku katika vyama vya ushirika vya wakulima hao mkoani Tabora.
IGP Mangu amemteua Kamishna wa Polisi Issaya Mngulu (pichani) ambaye ni
Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai hapa nchini kuongoza timu.
Timu hiyo ya upelelezi kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini
Dar es salaam tayari imewasili mkoani hapa kuanza kazi ya kuchunguza
ubadhirifu huo unaofanyika katika vyama vya msingi vya wakulima wa
tumbaku.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mara baada ya kuwasili mkoani
hapa Kamishna Mngulu alisema timu imeundwa kutokana na agizo la Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la tarehe 7/6/2014 alipokuwa
ziarani mkoani hapa baada ya kuguswa na kilio cha wizi mkubwa wa fedha
za wakulima wa tumbaku.
Kamishan Mngulu alisema timu hiyo ni maalumu na imekuja mahsusi kwa ajili ya
kuchunguza wizi wanaofanyiwa wakulima wa tumbaku kupitia vyama vya
msingi mkoani hapa
Alifafanua kuwa timu hiyo inaanza kazi mara moja kwa kuchunguza chama
kimoja hadi kingine ili kubaini wizi na hujuma zote zilizofanyika na
zinazoendelea kufanyika ambazo zimekuwa kero kwa wakulima wa zao hilo
katika mkoa wa Tabora.
‘Natoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Tabora kutoa ushirikiano kwa timu
hii mara watakapohitahika ili kuwezesha mafanikio ya kazi hii kwa
wakati mwafaka, kazi hii ni ngumu lakini tutaifanikisha kwa
ushirikiano wa wananchi na wadu wengine, aliongeza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...