Diamond Platnumz ni msanii mwengine mkubwa wa Kitanzania aliyejiunga na Mkito.com kwaajili ya kusambaza muziki wake mtandaoni. Msanii huyu anajiunga na wengine kama Fid Q, Nay Wamitego, Rich Mavoko, Vanessa Mdee, Juma Nature, Barnaba, Linah, Belle 9 na wengine wengi katika mchakato unaoendelea kuwawezesha wasanii kujipatia kipato kutokana na muziki wao kupakuliwa kwenye mtandao. Diamond kabla ya kuondoka kuelekea Afrika ya Kusini kwaajili ya video yake mpya aliona ni vyema kuungana na Mkito.com kwani ni kampuni ya Kitanzania yenye madhumuni mazuri kwa tasnia ya muziki nchini. Watumiaji wote wa Mkito.com sasa wanaweza kupata nyimbo za Diamond kupitia www.mkito.com ikiwemo albam ya Best Of Diamond na pia wimbo wake mpya Mdogomdogo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2014

    huyu dogo huko kujichora mwilini na swaumu atafunga na iswikhi kweli..?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...