Ili kuwa ni hafla ya aina yake iliyojaa tabasamu, kukumbatiana na maneno ya " welcome back, good to see you again, we have missed you" yakitawala wakati Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha- Rose Migiro alipofika Ofisini kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon na kisha kukutana na kubadilishana mawazo na Katibu Mkuu mwenyewe wakianza na mazungumzo ya faragha kati yao wawili na kisha kujumuika na wafanyakazi wa Ofisi Binfasi ya Katibu Mkuu na Ofisi Binafsi ya Naibu Katibu Mkuu. baada ya Mazungumzo yake na Katibu Mkuu, Dkt. Migiro pia alikutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu aliyemwachia kijiti Bw. Jan Eliasson.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akiwa na Dkt. Asha-Rose Migiro ( Mb) Naibu Katibu Mkuu Mstaafu na ambaye sasa ni Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakati alipotembeleza Katibu Mkuu jana Jumatatu. Hii ni mara ya kwanza kwa Dkt. Migiro kufika Umoja wa Mataifa tangu alipostaafu Unaibu Katibu Mkuu miaka miwili iliyopita. Kabla ya Viongozi hao wawili kupiga picha hii rasmi, walikuwa na mazungumzo ya faragha ( Tete a tete). Waziri Migiro yupo hapa Umoja wa Mataifa kuhudhuria Mkutano ulioitishwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu mchango wa Haki za Binadamu na Utawala wa Sheria katika Maendeleo Endelevu baada ya 2015.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na timu yake akiwa katika mazungumzo na Dkt. Asha- Rose Migiro ambaye alifuatana na Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi na Naibu wake, Balozi Ramadhan Mwinyi. Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu alisema, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amefanya jambo jema kumteua Dkt. Asha-Rose Migiro kwanza kuwa mbunge na kisha kumteua kuwa Waziri anayeshughulikia Sheria na Masuala ya Katiba, akasema uzoefu wake na mchango wake siyo tu kwamba ni muhimu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali ni muhimu pia katika Jumuiya ya Kimataifa. Ban Ki Moon alishindwa kuficha hisia zake pale aliposema mbele ya Maofisa wake kwamba siku zote amekuwa akimkumbuka Asha- Rose Migiro na kwamba amefurahi sana kwamba amepata nafasi yakufika Umoja wa Mataifa.
Ban Ki Moon akiagana na Dkt. Asha-Rose Migiro baada ya mazungumzo yao.
Baada ya kuagana na Katibu Mkuu , Naibu Katibu Mkuu Mstaafu Dkt. Asha-Rose Migiro alielekea ofisini kwa Naibu Katibu Mkuu Bw. Jan Eliasson ambako nako kulikuwa na kukaribisha na tabasamu za akina yake. na kisha wakawa na mazungumzo ya faragha.Pichani ni Naibu Katibu Mkuu, Bw. Jan Eliasson akimkaribisha kwa furaha Dkt. Asha- Rose Migiro ofisi kwake kwa mazungumzo.
Wakipata picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...