Wananchi wameshauriwa kufuata kanuni na taratibu sahihi za upatikanaji wa huduma za Maji ili kujiepusha
na utapeli unaofanywa na baadhi ya wananchi wachache wenye lengo la kuharibu utendaji kazi wa
dawasco na kuleta hasara kubwa kwa jamii.
Hayo yameelezwa na Afisa Uhusiano wa Dawasco Bi Everlasting Lyaro wakati wa maadhimisho ya wiki ya
Utumishi iliyofunguliwa rasmi jana jijini Dar.
Alisema kauli mbiu ya mwaka huu inaendana na dhima nzima ya utumishi uliotukuka unaoainsha misingi
na kanuni za utumishi ili kuimarisha utawala bora na uwazi sehemu ya kazi.
“Taratibu na kanuni sahihi za upatikanaji wa huduma ziko wazi kwa taasisi yetu kufuata taratibu sahihi
ikiwepo kufika ofisi ya dawasco iliyo kwenye kanda yake na kupewa fomu sahihi iliyo na maelezo binafsi
ya Mteja, na ikiwa mwombaji ni kampuni au shirika atatakiwa kuja na barua ya maombi iwe na muhuri wa
Shirika” alisema Lyaro.
Aliongeza kuwa taratibu hizo ziko wazi na wananchi wanapaswa kufika kwenye ofisi za Dawasco ili
kupunguza malalamiko wanayopokea baada ya kuhujumiwa na watu wachache wanaotoa huduma hiyo
kinyume na taratibu.
Aliwahakikishia wananchi kuwa mwombaji atarajie kuunganishiwa huduma ya Maji katika kipindi cha siku
14 hadi 21 baada ya kukamilisha malipo ya ada / gharama ya kuunganishiwa Maji.
Maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma yameanza rasmi wiki hii na kitaifa yamefunguliwa na Waziri
Ofisi ya Rais, Utawala Bora Mh George Mkuchika ikiwa na kauli mbiu ya “ Mkataba wa Msingi na kanuni
za Utumishi wa Umma barani Afrika ni chachu ya kuimarisha Utawala Bora na uendeshaji wa shughuli za
Serikali kwa uwazi”
Afisa Uhusiano wa DAWASCO,Bi Everlasting Lyaro (katikati) akitoa ufafanuzi wa shughuli na huduma zinazotolewa na DAWASCO kwa mwananchi aliyefika kwenye banda la DAWASCO wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma inayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Meneja wa huduma kwa mteja Bi Tumakwezi Sayi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...