KWA mara ya kwanza kwenye ukumbi wa Maisha Plus (Pilice Mess) kutafanyika tukio la aina yake la kumsaka Redds Miss Pwani 2014 usiku wa leo.
Katika Shindano hilo ambalo litakuwa ndiyo sehemu ya kuuzinduz ukumbi huo ambao leo hii ndiko kutakuwa na burudani kubwa ya muziki wa dansi kutoka katika bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Next level’ wakiongozwa na mzawa wa mkoa wa Pwani Ally Choki almaarufu kama ‘Mwarabu wa Kibaha’ ambao nao wameahidi kutoa burudani ya kihistoria kwenye onyesho hilo.
Bendi hiyo ambayo inatamba na vibao vingi ambvavyo vimeipa sika kama ‘Regina’ na nyinginezo.Mbali ya Choki ambaye atakuwa na kikosi chake kikali cha wacheza shoo kinachoongozwa na Mussa Hassan Nyamwela pamoja na wanenguaji wa kike kama Maria Soloma , Asha Said ‘Sharapova’ , Otilia na wengineo watanogesha na kuacha historia siku hiyo .
Katika shindano hilo jumla ya warembo Kumi watapanda jukwaani ambao Khadija Sihaba, Glory Jige, Irene Rajab, Mary Samwel, Arafa Shabani, Jeniffer David, Judea Joseph, Mary Mpelo,Roksana Msangi na Faith.
Mshindi wa Miss Pwani ndiye atapata nafasi ya kuuwakilisha Mkoa huo katika shindano la kanda ya Mashariki na baadaye katika fainali za Redd’s Miss Tanzania 2014.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...