Mwandishi mkuu wa Mbeya yetu Blog, Joseph Mwaisango
******

TONE MULTIMEDIA GROUP Ambao ni wamiliki wa Mtandao huu wa Mbeya yetu Blog , Tunapenda Kuungana na wadau wetu wote Kumpongeza Bwana Joseph Mwaisango ambaye ndiye Mwandishi Mkuu wa Blog hii ya Mbeya yetu  na Mmoja wa wakurugenzi wa Tone Multimedia Company Limited (TMCL)  ambao pia ni wamiliki wa Blogs za Mikoa TanzaniaTone Radio-Tz , This Day MagazineStay In Tanzania(Tanzania Tours) , Tone Tube Tz  , Matukio na Wanavyuo na Watanzania waishio nje ya Nchi kwa kutimiza miaka yake kadhaa siku ya Leo.

Tunapenda kumpa Hongera sana kwa kazi nzito ambazo anazifanya ili kuwaletea wadau habari zilizo sahihi na za uhakika zaidi kutoka pande zote za Mkoa wa Mbeya, Pia tunamuombea kwa Mungu ampe siku nyingi zaidi , Afya Njema na aendelee kuchapa kazi zaidi na zaidi bila kusahau kuongeza Ubunifu zaidi.

Pia katika Hili tunapenda kuwashukuru wadau Mbali mbali wa Habari wakiwemo Bloggers wote wa Tanzania, Magazeti, Radio na TV kwa kuendelea kuonesha ushirikiano mkubwa ili kazi ziendelee kwa ufanisi mkubwa

Mwisho tunapenda kumshukuru kila mmoja wetu ambaye ni mdau mkubwa wa Blog ya Mbeya yetu,  wote tupo pamoja katika kusherekea siku hii ya leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...