Serikali ya India imekabidhi msaada wa mashine ya kusafishia damu (hemodialysis) kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili yenye thamani ya dola 15,000 za Marekani. Akikabidhi msaada huo, Balozi wa India hapa nchini Bw. Debnath Shaw amesema mashine hii itasaidia juhudi za hospitali katika kutoa huduma za usafishaji damu. Bw. Shaw amesema Serikali yake itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania na wa Wadau wa Sekta ya Afya kwa kupitia Mpango wa Ubia (Public Private Partnership-PPP) ili kuboresha huduma za afya hapa nchini. 
Akipokea msaada huo, Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Agnes Mtawa amesema mashine hii imekuja wakati muafaka kwani zaidi ya  asilimia 60 ya wagonjwa wa figo  wanaotibiwa Hospitalini hapo wanahitaji huduma za usafishaji damu. Mashine hii itatumika kwenye chumba cha wagonjwa mahututi tu ili kusaidia waonjwa walilazwa  na wanahitaji huduma hiyo wakiwa hapo hapo ICU.

Alisema msaada wa mashine hii ya kusafisha damu katika wodi ya wagonjwa mahututi uliotolewa leo, umekuja wakati muafaka ambapo Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inatekeleza mkakati wake wa kuzidi kuboresha na kuimarisha huduma za afya hapa nchini na kitengo cha magonjwa ya figo ni eneo muhimu na hivyo huduma ziweze kutolewa kwa wakati, kwa wingi na kwa viwango vinavyokubalika. Huduma za usafishaji damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zilianzishwa rasmi mwaka 2011 chini ya idara ya tiba kwa lengo la kuboresha huduma kwa wananchi. Huduma hii ilipoanza,  Hospitali ilikuwa na mashine tano na  ambazo zimekuwa zikitoa huduma kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ikiwamo wagonjwa mahututi mabapo kwa sasa kuna mashine 16. 
“Pamoja na hayo, kumekuwepo na changamoto nyingi katika  kutoa huduma  za magonjwa ya figo pamoja na huduma ya usafishaji damu hapa nchini hususani katika Hospitali yetu ya Taifa Muhimbili ambazo ni pamoja na upungufu wa madaktari bingwa wa magonjwa ya figo. Tanzania ina wataalamu saba tu wa magonjwa ya figo na wengine watatu wapo masomoni wakimalizia masomo yao katika fani hiyo. Kwa hiyo unaweza kuona ni kwa jinsi gani tunahitaji wataalamu hawa wa kutosha ili kuweza kuhudumia watanzania wapatao milioni 45” alisema Bi. Mtawa. 
Bi. Mtawa ameiomba Serikali ya India kupitia Balozi wake hapa nchini isaidie kuanzisha mpango wa kubadilishana uzoefu (exchange programme) kati ya wataalam wa figo Muhimbili na wa India ili kuwapa fursa ya kubadilishana uzoefu katika kazi zao ambapo alisema kufanikiwa kwa zoezi hilo utawajengea uwezo zaidi na hivyo kuzidi  kuimarisha huduma husika hapa nchini.
Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Debnath Shaw akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi Agnes Mtawa wakati akiongea na vyombo vya habari.
Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Debnath Shaw akiongea na vyombo vya habari kabla ya kukabidhi msaada huo.
Mh. Balozi wa India nchini Bw. Debnath Shawa akikabidhi mashine ya kusafisha damu kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Agnes Mtawa
Dkt. Onesmo Kissanga daktari bingwa wa magonjwa ya figo akitoa maelezo kwa wanahabari hawako pichani  jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi.
Baadhi ya Wauguzi katika wa chumba cha wagonjwa mahututi ambapo mashine hiyo inatumika wakiwa katika picha ya pamoja wakifuraia msaada huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...