Alama ya chaki ya kupulizia (spray) ni moja ya ingizo jipya kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil. Tayari refa ameshaitumia mara ya kwanza kwenye mechi ya ufunguzi kati ya Brazil na Croatia usiku wa kuamkia leo, pale refa alipochora kwa kupulizia na kuweka alama wapi wachezaji wasimame wakati wa kupigwa mpira wa adhabu (pichani chini), ili kuthibiti zogo la wachezaji, ama wapi mpira uwekwe kabla ya kupigwa.
Chaki hiyo, ambayo huyeyuka baada ya dakika chache, ilianza kutumika mwaka jana kwenye kombe la Klabu Bingwa ya Dunia, ambapo huko Argentina na Brazil imetumika kwa misimu kadhaa iliyopita.
Pia ilitumika kwa majaribio katika michuano ya FIFA ya wachezaji walio na umri chini ya miaka 20 mwaka jana.
Je, huu ni mzigo wa ziada kwa refa ambaye sasa atabeba kalamu na notebook, filimbi, kadi ya njano na nyekundu, kidude cha kusikilizia masikioni na sasa kikopo cha chaki ya kupulizia kitachoning'inia kwenye mkanda wa kaptula yake.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...