Na Faustine Ruta, Bukoba.
Timu ya Kagondo FC imejipatia Alama tatu muhimu kwenye Mtanange wao dhidi ya timu ya Buhembe FC leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini kwenye Michuano ya Kombe la Kagasheki. Bao hilo la pekee lilifungwa na Mchezaji namba tisa Mgongoni Abduratif Khamis katika kipindi cha kwanza dakika 37.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa bao hilo 1-0 na kipindi cha pili timu zote mbili hakuna iliyoziona nyavu za mwezake timu licha ya kushambuliana mara kwa mara. Mwamuzi alipuliza kipenga dakika 90 kumaliza mtanange huo na Timu ya Kagondo FC wakiibuka na ushindi huo wa bao 1-0.
Mapema leo Mchana Timu ya Nshambya na Kibeta ziliumana na timu zote mbili zilimaliza mtanange kwa sare ya bila kufungana kwa kutoka 0-0. Kesho Ligi hii inaendelea tena kwa siku ya nne na kutakuwepo na michezo miwili, Mapema ni Nyanga vs Kitendaguro na Jioni saa 10:00 ni Wagonga Nyundo "Ijuganyondo Vs Kahororo".
Kikosi cha Timu ya Kagondo Fc
Kipute kilianza kwa Timu ya Buhembe kwa kasi sana.
Kwa picha zaidi za mwanalibeneke Faustine Ruta wa Bukoba BOFYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...