Wenyeji Brazil  wameanza michuano ya Kombe la Dunia kwa ushindi finyu wa mabao 3-1 dhidi ya Croatia usiku wa kuamkia leo  jijini Sao Paulo, na kuponea chupuchupu kutoka sare katika mchezo ulioanza kwa mabingwa hao mara tano kujikuta nyuma kwa goli moja la kujifunga wenyewe mwanzoni mwa kipindi cha kwanza. 
Nyota wa Brazil Neymar analalamikiwa kubebwa na refa Yuichi Nishimura kutoka Japan baada ya kuambulia kadi ya njano (badala ya nyekundu)  kwa kumpiga kipepsi kwa makusudi mlinzi Luka Modric wa Croatia mbele ya mashabiki 61,000. 
Dakika chache baada ya rafu hiyo na kadi ya njano, Neymar alisawazisha kwa mkwaju wa mita 25, kabla ya wenyeji kupata bao la pili, la penati (ya kubebwa), pale Fred alipojirusha ndani ya boxi baada ya kuguswa kidogo tu na mlinzi wa Croatia.
Oscar, aliyekuwa nyota wa mchezo, naye alifunga bao tamu la mchezo, kuihakikishia ushindi wa Brazil ambayo, hata hivyo, inatajwa  na wadadisi wa mambo kuwa inabwebwa na FIFA ambayo inasemekana inakutaka wenyeji washinde kombe hilo kwa hali yoyote ile.
 Hii inatokana na mbeleko tatu za wazi ambazo refa alionesha kuwabebea Brazil (kutomtoa Nyemar, kutoa penati kwa Fred kujirusha na kukataa bao la Croatia), kiasi hata makelele yanasikika kila kona kwamba Kombe la Dunia safari hii itakuwa na  mizengwe mingi kama ile iliyoiandama FIFA (ya tuhuma za rushwa kuipa Qatar wenyeji wa mashindano), na wadadisi wanasema ngoja tuone iytavyokuwa.





  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2014

    MImi sio mwandishi wa habari. Ila ninadhani unapoandika habari ambayo umeichukua sehemu, ni muhimu kutokuiandika kwa hisia maana sio wote watakao kubaliana nawe. Habari hii kaka Michuzi umeiandika kwa hisia zako kwa sababu tu hukutaka Brazil ishinde. Tayari nimefahamu kwamba wewe sio mshabiki wa Brazil na ukiendelea tu kuandika na kesho nitafahamu timu unayoshabikia. Achana na uandishi matope,andika kama mtu unayehudumia hadhira ya watu wote.

    Kaka.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2014

    Penalty yenye utata iliimaliza kabisa Crotia

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2014

    3-1 ni ushindi finyu? Hii ni Soccer, sio netball au handball! Na ikumbukwe mwaka 1990 Argentina alianza kwa kuchapwa 1-0 na Cameroun lakini akaenda mpaka fainali!

    Kwa mpenda Soccer, ni vizuri kuziba masikio na kuangalia kambumbu uwanjani, ikiwezekana zima (mute) sauti kwa TV yako, ndipo utakapoachana na siasa nje ya uwanja!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2014

    The game was perfectly managed.Even game analysts(kuffour,Giggs,Okocha,...)had fair comments on it.Michuzi's views seem to be personally subjective and don't reflect the majority of viewers'.Anyway it is difficult to hide hate and love.
    I remain.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 13, 2014

    Msiwe mnarukia mambo wakati wote hamkuwepo uwanjani na yote haya mnayaona kwa TV ama kusoma mitandaoni kama alivyofanya ankal na kutubandikia. Hebu pitia hii uone wanavyosema walio uwanjani

    http://www.dailymail.co.uk/sport/worldcup2014/article-2656584/Brazil-2-1-Croatia-Neymar-scores-twice-escapes-sending-hosts-start-win-Sao-Paulo.html

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 13, 2014

    Hivi mpaka umri huu hamjaweza kuangalia mpira na kufanya tafakuri yenu wenyewe? Mpaka msimuliwe?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...