MAREHEMU MWASHABAN A. LIGANJA
Mpendwa Mama,
Mama unatimiza miaka saba (7) sasa toka ututangulia mbele ya haki. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa muda wote uliokuwa nasi. Si tu kuwa Mama bali pia kuwa mtu wa pekee miongoni mwetu Mama. Ulibarikiwa mambo mengi ambayo tukianza kuyaorodhesha hapa tunaweza kujaza kitabu ila kwa ufupi UPENDO usiokuwa na kipimo.
Mama DAIMA utakumbukwa na Mumeo Mpendwa George Mapango, wanao Mariam (Chuma), Eva (Hawa), Jackson (Kibabu), Patrick (Said), Richard na watoto wote kwa upande wa Dada zako na kaka zako. Mkweo Deogratius Sakawa, Wajukuu zako Precious (P), Pricilla na Jasmine. Wadogo zako, Ndugu, Jamaa, Marafiki zako, Majirani na Wafanyakazi Wenzako.
Tutaendelea kufuata ushauri wako na mema mengi uliyotufundisha. Kwa upendo wako unatuunganisha familia na tutaendelea kukumbuka busara zako na hekima daima.
KISOMO KITAFANYIKA LEO TAREHE
07 JUNI, 2014 SAA 04.00 ASUBUHI.
07 JUNI, 2014 SAA 04.00 ASUBUHI.
INNA LILAH WAINA LILAH RAJIUUN
Mafundisho yako tutayaishi milele. Juzi nilisoma diary yako nikahisi nimeongea na wewe. Niliisikia sauti yako moyoni mwangu,Mama.
ReplyDeleteDaima tutakukumbuka huku tukiwa na tumaini la kuwa siku moja kuonana nawe. We will always cherish good memories and time we shared together.
R.I.P Mama.
Mariam Chuma (Dachu).