KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MAMA YETU MPENDWA MRS K. MNUBI
sasa ni miaka miwili tangu mama yetu kipenzi ulioitikia sauti ya Mungu hapo tarehe 07.06.2012.
Sisi kama familia tunatoa shukrani za pekee kwa Mungu kwa jinsi alivyoweza kutulinda na kutupa
Faraja ya pekee katika kipindi chote cha majonzi na hadi sasa tunatimiza miaka miwili bila kuwa
nawe. Tunakukumbuka sana mama japo kimwili haupo nasi, pengo lako daima haliwezi kuzibika.
Tunakukumbuka kwa upendo wako, ushauri wako kama mama na mke. Kipekee unakumbukwa sana
na mume wako mpendwa Kedmond, watoto wako Catherine, Restituta, mama ako mpendwa na ndugu
jamaa na marafiki.
Dua ya kumuombea marehemu itafanyika nyumbani kwake Msamala, Songea tarehe 07.06.2014
INNALILAHI WAINA ILLAIHI RAJIUUN.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...