Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mh.Prof Anna Tibaijuka akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wadau mbalimbali kwenye jukwaa la Uwekezaji katika Sekta ya Nyumba.Prof.Tibaijuka alisema kuwa Serikali inaridhishwa na utendaji unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Alisema katika kipindi kifupi Shirika limefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya makazi na kwamba miradi hiyo itakapokamilika,itaifanya miji hiyo kuwa ya kisasa.Prof.Tibaijuka alisema kuwa kampuni za uwekezaji kwenye sekta ya nyumba ni muhimu na hunyanyua uchumi wa nchi,alisema kuwa ili Taifa liweze kuendelea ni lazima liwe na mipango miji na kwamba kupanga miji sio kukata viwanja bali ni kunahitaji mambo mengi.Prof Tibaijuka amewataka wananchi kuwa tayari katika suala la kupanga miji,na maeneo yote yatakayopangwa ni lazima yafidiwe.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Nehemia Mchechu akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wadau mbalimbali kwenye jukwaa la Uwekezaji wa sekta ya nyumba lililofanyika jijini Dar.Bwa.Mchechu alisema kuwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),limedhamiria kuyabadilisha maeneo ya jiji la Dar na mikoa mingine nchini baada ya kuzindua ujenzi wa miji midogo.

Alisema kuwa Miradi hiyo itakapokamilika itabadilisha mandhari ya maeneo mbalimbali nchini na kuyafanya kuwa ya kisasa,Mchechu alisema kuwa wataanza na miradi mitatu ikiwemo miji midogo katika majiji ya Dar es salaam na Arusha na kuendeleza nyumba zao zilizobomolewa.

Alisema kuwa katika jiji la Dar,watakuwa na mradi wa salama Kigamboni na Kawe mbayo italifanya jiji hilo kubadilika kuwa la kisasa,aliongea kuwa katika miradi hiyo,kutajengwa nyumba nyingi za kuishi, biashara na sehemu za huduma muhimu .

Mchechu amesema kuwa mradi mwingine utakaotekelezwa ni wa Usa River Safari City utakaojengwa jijini Arusha,ambao utalenga kulibadilisha jiji hilo na kuwa la kisasa,aliongeza kusema kuwa mradi huo utagharimu dola za Kimarekani bilioni mbili (zaidi ya shilingi bilioni 3.4) na itakamilika kati ya kipindi cha miaka saba mpaka 12.Bwa.alisema kuwa miradi mingine ambayo itatekelezwa ni pamoja na  Bagamoyo,Dodoma,Mbeya,Mtwara,Lindi,Mwanza na maeneo Mengine.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Bi.Zakhia Meghi akizungumza kwa ufupi mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wadau mbalimbali kwenye jukwaa la Uwekezaji wa sekta ya nyumba.
Sehemu ya meza kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye jukwaa hilo la uwekezaji wa sekta ya Nyumba,lililofanyika jijini Dar
Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye kwenye jukwaa la Uwekezaji wa sekta ya nyumba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2014

    Sisi wote niwatanzania leongo la Baba wa taifa kuhusu shirika la nyumba la Taifa ilikua ni kuwasidia watu wa kipato cha chini kuweza kupata makazi.chakushangaza hizi nyumba wamejaa wahidi tu ukifatilia hupati wanatangaza nyumba zipo . mchango wangu ni kwamba naomba wanapokua wanazidua nyumba mpya wawa lenge kwanza watu wa kipato chaa chini sio matajiri hilondio lengo la baba wa taifa ,

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2014

    Ili bei za nyumba ziende chini NHC ipewe ushindani, vijana magraduates wa architecture, civil enngineering na electrical engineering waingie kwenye vikundi vya kuanzisha kampuni za ujenzi wawezeshwe kupwewa mikopo nao wajenge nyumba nikoani na sejhemu nyingine, bei yao ikiwa nzuri NHC watashusha nao bei.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 26, 2014

    It looks political!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 26, 2014

    Cha Kushangaza ni kwamba kila wanapopanga mipango miji jina la Dar es salaam,lazima liwepo.ningeshauri kuwa miradi ya mipango miji lazima ilenge katika kuwapa haki wenyeji wa asili wa eneo lile,sio kuwandoa wenyeji wakazi na kuwapa nyumba au viwanja wageni,makosa haya mara nyingi yanafanya na Wizara usika.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 26, 2014

    Miradi hii ilenge nje ya Dar-es-salaam,kama vile Chalinze,Bagamoyo na kungineko hapa Dar,tumeshachoka kufukuzwa kijanja na maeneo yetu wakapewa wageni kwa visingizio vya miradi hii ya ujanja ujanja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...