Leo
hii Ijumaa Juni 20, 2014, kuanzia saa 5 mchana kwa saa za Marekani na saa 12
jioni kwa saa za Tanzania nimegundua kwamba akaunti yangu binafsi ya barua pepe
kidundo2001@yahoo.com
imevamiwa na wahalifu.
Nimechukuwa hatua stahili na za haraka katika
kushughulikia tatizo hili. Naomba kuwashukuru wote walionitanabahisha kwa
kufahamu kwamba niko Washington DC, Marekani,
na wakashangazwa kupokea barua pepe nyingi ambazo zimedai kwamba niko
Nassau, Bahamas, Manila Philippines, Rio de Janeiro, Brazil na Singapore na
kwamba nimepata matatizo ya kuvamiwa na majambazi na kuibiwa kila kitu na hivyo
kuomba msaada wa dharura.
Naomba kuchukuwa fursa kutoa taarifa hii kwamba mimi niko salama Washington DC,
Marekani, na ninaendelea na shughuli zangu za kazi katika Ubalozi wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania bila ya matatizo yeyote. Pia naomba mtu yeyote atayepata
email kwa anuani hiyo aipuuze, si ya kweli. Nitatoa tena taarifa mara
nitapokuwa na anuani yangu halisi muda si mrefu ujao.
Namshukuru Ankal Muhidin
Issa Michuzi kwa kunitumia taarifa ya kwanza kuhusiana na uhalifu huu, na kunishauri kuchukua hatua haraka.
Suleiman
Saleh
Washington
DC
Juni
20, 2014
haya matatizo hujitokeza sana kwa accounts za hotmail na yahoo
ReplyDeletejaribu kutumia gmail zaidi pamoja na kuweka password ngumu yenye numbers na herufi kubwa na ndogo ukiweza