Serikali imeshauriwa kuweka mgawanyo sawa ya utekelezaji katika miraji ya Maji nchini ili kuondoa tatizo sugu la Maji kwa maeneo yenye ukame na upungufu mkubwa wa Maji.
Akichangia wakati wa bajeti ya Wizara ya Maji, mbunge wa Singida Mashariki Mh Tundu Lissu alisema imefika wakati serikali lazima iweke uwiano sawa wa mgawanyo wa fedha za miradi ya maji kwenye mikoa na sehemu zenye upungufu mkubwa wa Maji hapa nchini.
Akitolea mfano jimboni kwake alisema bajeti ya mwaka huu kwa jimbo lake la Singida Mashariki jumla ya Milioni 839 zimetengwa kwa ajili ya jimbo lake. Alipongeza serikali kwa miradi miwili ya Maji iliyoanza kutekelezwa jimboni kwake katika wilaya ya Ikungi na Mungwaa na kwamba ukarabati wa visima vilivyojengwa na taasisi ya Catholic Service Relief (CSR) ukiendelea.
Aliongeza kuwa kwa mikoa yenye vyanzo vya Maji kama vile Mito na Maziwa ni muhimu fedha kidogo zikatumika na nguvu nyingi ikaelekezwa kwenye maeneo yenye ukame mkubwa wa Maji kama vile Singida, Dodoma, Shinyanga na Simiyu.
Mbunge wa Singida Mashariki, Mh Tundu Lissu akichangia hoja ya wizara ya Maji wakati wa Bajeti ya Makadirio na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2014/2015.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...