Huo msalaba uuonao hapo ni taa za magazri zilizo katika foleni mishale ya saa moja jioni kwenye makutano ya barabara za Morogoro road na Nelson Mandela jijini Dar es salaam. Hakika kuna haja ya kutafuta njia mbadala za kupunguza foleni ya magari katika jiji hili. Ushauri wa bure kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Madiwani wa Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni. Boresheni njia za pembeni ili magari yaweze kupungua katika barabara hizi kuu.
Picha na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii
Picha na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii
Hivi nikirudi bongo vacation nikipanda bus au nikitembea kwa miguuu mtanicheka? Watu wa salendar bridge,upanga ,laibon ,Ada estate tembeeni kwa miguu kwenda mjini.mimi Nakaa I swear nitatembea kwa miguu I won't care foleni siwezi kabisa very stressful hapa USA penyewe tu foleni kidogo tu Kichwa kinaniuma nisije pasta anxiety .I will walk
ReplyDeleteTypical Tanzanian.. Hivi we anony hapo juu unadhani Wabongo wa leo ni washamba kiasi hicho hata wakae wapoteze muda wao kuangalia we unafanya nini? Tembea hata kwa tumbo uone kama atayekumaindi.
ReplyDeleteWe jamaa mkali kweli, ukawasha kadenge kako huyooo mpaka Ubungo mataa! Asante kwa picha hizi siku nyingine nikupe company kama hutojali.
ReplyDeleteMimi niko na mtazamo tafauti.
ReplyDeleteJamani watanzania tumezidi kuekeza kwenye siasa. tumejawa na akili za kisiasasiasa tuu na akili zetu zimeganda kwamba bila CCM au bila upinzani hatuwezi kuwa na maendeleo....tuamue jamani kuachana na kuekeza kwenye politics.kilachama kaziyake imekua ni kuumiza kichwa kutafuta sare zake na mbinu za kushinda tu na tukimaliza chaguzi fulani tunaandaa nyengine "life goes on"tukishaweka bomba ya maji au kujenga banda la shule tunasema tumepata maendeleo na tunajisifu na kufunga mikono. Wenzetu hayo wamepita zamani sasa wanafikiria "drones"-ndege zisizo na rubani.Sisi bado tusaka mkate wa siku moja jamani!!! KWA MIUNDO MBINU hii ya barabara ukweli hapa asia nilipo mpaka kwa barabara za vijijini kwa wakulima flyovers(barabara za juu) ni kitu cha kawaida tu,msongamano barabarani upo lakini haufanani na wa nyumbani hapo...tumezidi jamani,viongozi wakijahuku pia wanaona hayo.Nashindwa kuamini kwamba tunashindwa kueka flyover moja hapo ubungo au round about na nyengine fire pale kweli? Foleni yote dar itaisha 100%. Hatujakuwa watu wengi sisi kama hawa, hatuna magari mengi sisi kama hawa. Siwezi kuamini kwamba eti ni kuongezeka idadi ya watu au watumiaji,yaani wenye magari wameongezeka...sio kweli hata kidogo. Ni ukosefu wa mbinu bora za kisasa kama wenzetu hapa.Na ni mbinu tu sio utajiri kwani mipango halisi na umakini wa uhakika hauhitaji uwe tajili.Ka-flyover kamoja hapo ubungo ni garama za kampeni tu za uchaguzi. Jamani tuachane na politics zisizona manufaa.tujenge nchi yetu. nchi ikishajengeka vizuli no chadema,no nccr, cuf no ccm sote tutanufaika na kutembea kifua mbele. Wadau wa kisiasa acheni kulumbanalumbana au chuki au kulaumiana tujenge nchi yetu kwanza bado hatujafanyakitu."nchi ndogo tu duniani zinatengeneza drones sisi bado tunalumbana na kujisifu kwa kupata mkate tu...shame"