Wachezaji wa Spain wakitoka nje ya uwanja baada ya kuvuliwa ubingwa wa dunia na kufungashiwa virago na Chile (chini)
Na Sultani Kipingo
Usiku wa kuamkia leo ulikuwa wa aina yake huko Brazil. Utawala wa Wafalme wa Kombe la Dunia, Spain, uliota mbawa. Mchezaji wa Australia alifunga goli la mwaka, na Mfalme Willem-Alexander na Malkia Maxima wa Uholanzi walisisimkwa mno kuona nchi wanayoongoza ikipiga hatua mbele kuelekea Ubingwa kiasi hata wakapozi picha za selfie na Arjen  Robben, Robin van Persie na wenzao kwenye chumba cha kuvalia.

Siku ya saba ya michuano hii ilainzia mji wa Porto Alegre. Ikaishia takriban maili 2000 kutoka hapo (naam, Brazil kubwa ati), Ambapo Uholanzi na Chile wakapata tiketi kuingia raundi ya 16 bora na mchezo mkononi. 
Hapo Australia, Spain na Cameroon ndio wameshafungashiwa virago, huko Croatia ikiwa imeshinda vizuri kujiweka katika kinyang’anyiro cha utatu na Brazil na Mexico kuwania tiketi mbili za kuingilia hatua ya mtoano. 
Kituko cha siku kilikuwa wakati wa mchezo wa Cameroon na Croatia ambapo katika dakika za majeruhi huku wakiwa chini kwa bao 4-0, beki wa Cameroon Benoit Assou-Ekotto   alimpiga kichwa mchezaji mwenzie Benjamin Moukandjo (kushoto). Na hasira za kufungwa za Assou-Ekotto ziliendelea mpaka chumba cha kuvalia baada ya kipyenga cha mwisho   na kumlazimu Samuel Eto'o  aingilie kati. 

Kituko kingine kilitokea wakati wa mchezo wa Chile na Spain, baada ya mashabiki wa Chile kuvunja uzio wa uwanja wa Maracana na kuvamia uwanja kupitia sehemu ya wanahabari wakijaribu kuingia uwanjani kuangalia mechi. 
Serikali ya Brazil imeamua kuwatimua mashabiki hao wapatao 85 na kuwapa masaa 72 kuondoka nchini humo kwa kuvamia uwanjani na kuwaparaganya waandishi wa habari ambao ilibidi watoke mbio kwa tukio hilo la aina yake katika Kombe la Dunia.

Matokeo: 

Australia 2-3 Netherlands 
Spain 0-2 Chile

Cameroon 0-4 Croatia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2014

    Hivi toka tupate uhuru Tanzania iliwahi kusogelea au kufikia kombe la dunia hata wakati mmoja?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2014

    Hivi toka tupate uhuru Tanzania iliwahi kusogelea au kufikia kombe la dunia hata wakati mmoja?

    Kwani ni lazima?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...