Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimpongeza Rais mpya wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika baada ya Rais huyo mpya wa Malawi kukabidhiwa madaraka jijini Brantyre kwenye hoteli Sunbird. Baada ya kukutana viongozi hao walipata fursa ya kuzungumzia masuala la kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili na kukubaliana kuendelea kuwa na mahusiano mema kama nchi zinazoishi ndugu na jirani. Picha kwa Hisani ya Ikulu ya Malawi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DkT. Mohammed Gharib Bilal leo Jumatatu Juni 02, 2014 ameshiriki katika sherehe za kukabidhi madaraka kwa Rais mpya wa Malawi Profesa Arthur Peter Mutharika katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Kamuzu Banda, jijini Blantyre.
Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Rais wa Botswana sambamba na wawakilishi wa nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini na nyinginezo.
Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Rais wa Botswana sambamba na wawakilishi wa nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini na nyinginezo.
Akihutubia baada ya kukabidhiwa sime ambayo ni ishara ya kuwa kiongozi wa watu wa Malawi, Rais Mteule Mutharika alisisitiza kuwa, katika kipindi cha utawala wake atahakikisha kuwa anaifanyia makubwa Malawi sambamba na uhakikisha kuwa anaifanya Malawi itimize majukumu yake ya kimataifa kufuatia kutambua kuwa kujitenga kunaweza kuifanya Malawi kutonufaika na fursa zilizopo duniani.
“Nchi hii ipo katika dunia na siyo rahisi tena kuwa na fikra kwamba Malawi inaweza kubaki peke yake kama kisiwa. Tunahitaji kuwa na wenzetu wa kusaidia maendeleo ya Malawi.
Tunawahitaji wahisani toka Kusini ama Mashariki, tunayahitaji mataifa tajiri na mataifa yanayoendelea. Tutafanikiwa sana kama tutaendeleza urafiki kwa wote. Tufanye hivi bila kujali kuwa sisi ni taifa kwani hali ya sasa inahitaji kila mmoja wetu kushirikiana na mwenzake,” alisema.

Katika hotuba hiyo pia amesisitiza kuwa kipindi chake cha utawala atajitahidi kukabiliana na rushwa na kwamba hatakuwa na mchezo kwa wala rushwa katika kipindi akiwa madarakani. Pia alisisitiza kuhusu umuhimu wa kuiunganisha Malawi kwa miundombinu bora ili kuboresha maisha ya wananchi sambamba na kusogeza huduma za wananchi karibu.
Rais Mutharika aliapishwa juzi baada ya kuwashinda washindani wake akiwemo Rais aliyemaliza kipindi chake Joyce Banda ambaye hata hivyo hakuweza kutokea katika sherehe hizi za kukabidhi madaraka.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal na msafara wake walitarajiwa kurejea nyumbani leo hii Jumatatu mara tu baada ya kukamilika kwa kazi hii ya makabidhiano.
Ankal, msaada tutani maana historia tunamjua Mzee Kamuzu Banda tu
ReplyDeleteHasting Kamuzu Banda alizaliwa 1898 na kufariki mwaka 1997 akiwa na miaka 99.
Swali huyo Rais Mstaafu Kamuzu Banda aliyeshiriki kuapishwa kwa Mh Rais Prof . Mutharika ni Kamuzu yupi?
Mdau
Christos Papachristou
Diaspora
Ankal nami uhudhurio wa Rais wa zamani Kamuzu Banda unanitia hofu kwani huyu mzee alishapita kipindi hapa Duniani. Au mzimu wake huo?
ReplyDeleteNi kamuzu unaemjuwa wewe ili kaja tofauti, kimzukamzuka.
ReplyDelete