Kocha mkuu wa zamani wa timu ya Taifa, taifa Stars Marcio Maximo 
amesaini mkataba  wa kuwa kocha mkuu na timu ya Yanga kwa muda wa 
miaka miwili. makubaliano hayo yamefikiwa jana, wakala  anaye 
mwakilisha Ally Mleh wa kampuni ya Manyara Sports Management 
amethibitisha hilo.

"Ni kweli kocha Marcio Maximo amekubali kuingia mkataba na timu ya  Yanga ambapo anatarajiwa kuanza kazi rasmi tarehe 27/06/2014 ambapo  atafuatana na msaidizi wake Leonardo Neiva. Mazungumzo ya makubaliano   hayo yalichukua muda mrefu kidogo hatimaye tumefikia
makubaliano.Tunashukuru mungu kila kitu kimekamilika.

Kwa niaba ya Marcio Maximo napenda kuushukuru uongozi wa klabu ya
Yanga, shukrani za pekee kwa mwenyekiti wa Yanga ndg Yusuf Manji na
makamu wake Clement Sanga,  kwa kweli wameonyesha  umakini na
professional kwa muda wote wa  majadiliano. Nawaomba
wachezaji,wanachama na wapenzi wote wa yanga tumpe ushirikiano.

Baada ya kumaliza mkataba wake wa kuifundisha Taifa Stars nchini
aliingia mkataba na timu kubwa nchini brazil  mpaka mkataba wake
ulipoisha.Kwa wakati huu kulikuwa na mazungumzo na timu mbalimbali
Zilizotoa  ofa nchini China, Ethiopia na Afrika kusini lakini Yanga
wamefanikiwa kumnasa kocha huyo.

Maximo anatarajia kuwasili kesho siku ya Alhamis saa saba mchana

 
Maximo ilikuwa awasili nchini baada ya fainali za kombe la dunia lakini kutokana na mkataba alioingia na Yanga imebidi afupishe mkataba wa kazi ya 'commentator' aliyokuwa akiifanya nchini Brazil ili awahi kuandaa program zake Yanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2014

    Aje achape kazi. Mimi ni mpenzi wa Simba, lakini si vibaya nikisema kuwa kama Yanga watapata mafanikio makubwa chini yake,na inatokea nafasi ya ukocha Stars basi si vibaya akapewa tena timu ya Taifa. Lakini Yanga ikidorora basi tujue huyu zilipendwa tena.- Kilakshari

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...