Sehemu ya Wacheza Filamu nchini waliokuwa wamebeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu George Otieno Okomu (George Tyson) wakijipanga tayari kwa akili ya kuongoza shughuli ya Kuga mwili iliyofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.Mwili huo umesafirishwa kupelekwa nchini Kenya ambako ni nyumbani kwao na Marehemu kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Jumamosi ijayo baada ya kukamiliza kwa mipango yote.Picha zote na Othman Michuzi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Saddick akiwaongoza waombolezaji mbali mbali kwenye shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu George Otieno Okomu (George Tyson) waliofika kwa wingi kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi Mkuu wa Kipindi cha The Mboni Show,Mboni Massimba (kulia) akiwa ni mwenye huzuni sana kwa kuondokewa na Mwaznilishi mwenza kwa Kipindi chake hicho ambaye alifariki Dunia katika ajali ya Gari huko Mkoani Morogoro wakati wakitokea Mkoani Dodoma kukabidhi msaada wa Madawati katika moja ya shule za msingi zilizopo mkoani humo ikiwa ni maadhimisho ya Miaka miwili ya kipindi hicho.

Aliekuwa Mke wa Marehemu George Otieno Okomu (George Tyson),Yvone Chelly (Monalisa) na Mwanae Sonia wakiwa ni mwenye Majonzi makubwa kwa kuondokewa na mpendwa wao.Kushoto ni Mama wa Monalisa,Bi. Natasha.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Saddick akitoa nasaha zake wakati wa msiba huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...